Jumamosi, 4 Januari 2014

MKUMBUKE KATIKA MAOMBI MWIMBAJI HUYU WA NG'ANG'ANIA SHINYANGA


Getruda Ngassa akiimba na wenzake wa AIC Shinyanga walipokuwa mkoani Dodoma wakati wa Krismasi.
Hii ni kwa wote wakristo na wapenzi wa muziki wa injili, mkumbuke mama Getruda Ngassa mwimbaji nyota na solo wa kwaya maarufu ya AIC Shinyanga wana wa ng'ang'ania baraka za BWANA ambaye amelazwa katika hospitali ya Amana Ilala jijini Dar es salaam kutokana na tatizo la presha ya kushuka(Low Blood Pressure).
Ambapo kwa mujibu wa katibu wa kwaya hiyo Gody Magulu kupitia ukurasa wao wa Facebook amesema hali ya mwimbaji huyo ilikuwa mbaya siku ya kujana hadi kufikia kupumulia mashine, lakini Mungu ni mkuu kwani jioni ya jana na leo asubuhi hali yake ilikuwa ya matumaini.

Kwaya ya AIC Shinyanga walikuwa mjini Dodoma wakati wa sikukuu ya Krismasi kisha kuingia jijini Dar es salaam kuwasindikiza waimbaji wa AIC Chang'ombe vijana choir (CVC) ambao walikuwa wakitimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kwaya yao huku Getruda akiwa ni mmoja wa waimbaji waliongozana na waimbaji wengine wa Ng'ang'ania katika msafara huo.

www.mwakasegeinjili.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni