Alhamisi, 16 Januari 2014
FAMILIA YAUZA KILA KITU ILI KUMUHUBIRI KRISTO KWA MASIKINI
George, mkewe na watoto wao ©indiegogo
Familia ya bwana George na mkewe Vonda Sisneros yenye jumla ya watoto wanne ambao walikuwa wakijishughulisha na shughuli mbalimbali za kujipatia kipato huko nchini kwao Marekani, mume akimiliki kampuni ya usafi pamoja na usafishaji wa mazuria huku mke akiwa ni msanii anayejishughulisha na uchoraji wameamua kuuza mali zao zote ili kuwa wamisionari wa kuhubiri habari njema za Yesu huko Guatemala.
Akizungumza na mtandao wa Vaildaily bwana George ambaye wameamia Guatemala toka July 2012 amesema wamemiliki vitu vingi sana duniani lakini hata hivyo hawakutosheka navyo, walinunua watakavyo lakini vilionekana kutowatosheleza. Kutokana na imani yao kwa Mungu wakaamua kuuza vitu vyao vyote zikiwemo biashara zao zenya mafanikio, nyumba na kuamua kufungasha na kuhamia Guatemala ambako watu ni masikini sana ambako mauaji hutokea kwa asilimia 99.5 kwa wiki.
George alifunga safari ya kwanza kabisa mwaka 2011 kwenda kutembelea kituo cha watoto yatima huko Guatemala kabla hajauza vitu vyake ambako anasema alisikia sauti ya Mungu ikimwambia hapo ndipo anapotaka awepo, anasema hakukuwa na mvumo wowote kutoka sehemu nyingine bali ilikuwa ni yeye na Mungu. George anasema kama ilivyo kwa baadhi ya vitabu unaposoma habari zilizomo kabla ya mwisho unataka kubashiri mwisho wake utakuwaje ndivyo hata yeye alikuwa akijisikia hivyo kwakuwa hakujua itakuwaje mwisho na familia yake.
George na familia yake tayari wameshakaa miezi 18 Guatemala pamoja na watoto wao Samuel (10), Gabriel (11), Cecilia (13), pamoja na Demar (22) ambaye anasoma chuo kikuu cha Colorado anapokuwa hayupo Guatemala. George (47) anasema walikuwa wanaishi maisha ya kifahari Colorado biashara yao ili shamiri wakati ambao kulikuwa na mtikisiko wa kiuchumi, walikuwa wakiishi maisha waliyokuwa wakiyaota kuishi nchini Marekani lakini wakawa wanahisi kama mlango unafungwa, kwa maana kadri ya vitu walivyokuwa wanamiliki na ndio walikuwa wakifanya kazi zaidi ili kuweza kulipia mali zao kitu ambacho amesema vile unavyofanya kazi zaidi na ndivyo vitu vingine muhimu vinakupita kando kama familia na Mungu.
Tangu wameanza kujitoa katika huduma hiyo George na mkewe wameshatoa pea za viatu zaidi ya 100, mtambo wa kuchujia maji safi ya kunywa zaidi ya 25, wamesaidia ujenzi wa jiko jipya la shule, jiko la mbao la kuchemshia maji ya kunywa na sasa wapo katika ujenzi wa kumjengea nyumba mama mwenye watoto wanne wakiume ambao wamekuwa wakilala nje sakafuni kwa zaidi ya miaka 11 iliyopita.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni