Ijumaa, 10 Januari 2014

ANGALIA VIDEO KWANINI KANISA LA GWAJIMA HAWAJAMUOMBEA AMINA CHIFUPA KURUDI HAI


Marehemu Amina Chifupa Mpakanjia ©CloudsFm.
GK imefanikiwa kuiona video hii ambayo mchungaji Josephat Gwajima mwanzilishi wa kanisa la Ufufuo na Uzima Duniani likiwa na makao makuu yake viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es salaam, akifafanua kwanini hawajamuombea kumrudisha duniani aliyekuwa mbunge wa viti maalumu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtangazaji wa kituo cha Clouds Fm cha jijini Dar es salaam, Tanzania marehemu Amina Chifupa Mpakanjia.

Angalia video hii akielezea kwanini hawakufanya hivyo kama watu walivyokuwa wakitaka kanisa hilo kuomba ili Amina arejee duniani, ikiwa pamoja na binti aliyeshuhudia kuwa na Amina huko walikochukuliwa msukule ambako binti huyo anadai alimwacha Amina akilima shamba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni