Hii ni habari njema kwa wapenzi wa kwaya ya Tumaini Shangilieni ya mkoani Arusha pamoja na wapenzi wa nyimbo za injili kwani kwaya hiyo ipo bize kwa wakati huu ikiendelea na kurekodi video yao mpya ya tano kutoka katika album yao ya "Nisamehe" ambayo video yake walianza kurekodi nchini Afrika ya kusini walipotembelea mwishoni mwa mwaka jana.
Video hiyo ikikamilika itakuwa ni video ya tano ya kwaya hiyo ambayo ilitamba na video yao ya kwanza inayoitwa Shangilieni na kufuatiwa na Shangilieni part 2, video ya tatu Unishike huku video ya nne ni ya nyimbo za matumaini (Tenzi za Rohoni) ambayo walirekodi live na sasa wanaandaa ya tano itakayoitwa "Nisamehe.
Mambo yakipamba moto, hapana shaka wimbo huu ni Nisamehe |
Baadhi ya wababa wakirekodi wimbo wenye mahadhi ya mkoa wa Tanga, kama ilivyoada ya Tumaini mdumange haukosi. |
Inapendeza kwakweli. |
Wakielezana jambo kabla hawajaendelea na rekodi. |
Hii ilikuwa nje ya majengo ya serikali mjini Pretoria Afrika ya kusini walipotembelea mwishoni mwa mwaka jana ambako ndiko walikoanzia kurekodi video hiyo. ©Samuel Kusamba. www.mwakasegebibilia.blogspot.com |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni