Jumatano, 15 Januari 2014
LIPO KUNDI KUBWA LA WATU WALIOCHANGAMANA NDANI YA WOKOVU.
Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe...
Nimejaribu kujizuia nisiseme hivi lakini nimeshindwa kujizuia,ni bora leo niseme tu kwa watu wote maana injili yapaswa kuhubiriwa,na kwenda kote katika mataifa,na hiyo ndio kazi tuliyopewa maana maandiko yanatuambia;
"Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; '' Mathayo 28:19
Kundi kubwa la watu hawa hawana na tofauti ya MPINGA-KRISTO,sababu
Maana halisi ya mpinga-Kristo ni yule anayejifanya Kristo hali si Kristo.
Au ni yule ajifanyaye mlokole ingawa si mlokole,
Kundi hili lipo leo hii makanisani mwetu likijifanya ni wa-Kristo hali wao si wa-Kristo. Kwa nje watu hawa huonekana ni watu wa rohoni lakini ukweli si watu wa rohoni,wanafanana na wapinga Kristo.Ngoja tusome maandiko,tuone yanasemaje juu ya hili nilisemalo hapa;
'' Na kundi kubwa la watu WALIOCHANGAMANA mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng'ombe, wanyama wengi sana. ''Kutoka 12 :38
Kipindi ambacho wana wa Israeli wanatoka huko Misri,hawakutoka wao kama wao tu.Bali walitoka na kundi kubwa la watu waliochangamana nao.
Hawa waliochangamana nao,walisafiri kama vile walivyosafiri wana wa Israeli.
Huwezi kuwatambua kwa macho ya kawaida watu wa namna hii waliochangamana.
Kanisa la leo halina tofauti na wana wa Israeli walipokuwa wakitoka Misri kwenda nchi ya ahadi.
Sababu tupo safarini,
tena hapo mwanzo tulikuwa Misri,lakini sasa tumetoka huko,Lakini katika kutoka kwetu lipo kundi kubwa la watu WALIOCHANGAMANA NASI katika safari ya kuelekea KANAANI.
Kanisa la kwanza lilikuwa ni kanisa la kushambulia,
Kanisa la leo ni la kushambuliwa.
Sababu ya uwepo wa MAKRISTO WALIOCHANGAMANA KATIKA SAFARI HII. Tuonapo haya tusishangaye sana maana yatupasa kujua ya kwamba si wote ni wakristo bali wengine ni kundi lililochangamana.
Biblia inatuambia vizuri sana,
ya kwamba kundi hili lililochangamana sio kundi dogo la watu bali ni kundi kubwa sana,na kundi hili lilikwea pamoja nao wana wa Israeli,ikiwa na maana kwamba kama wana wa Israeli walipotoka walimuimbia Mungu wao,basi na kundi hili nalo liliimba wimbo ule ule,
hata ikiwezekana na sauti ile ile,kama itakuwa ni sauti ya kwanza basi wote waliimba sauti ya kwanza,
Lakini tofauti ilikuwa ni UPAKO,ambao hautafanana kamwe.
Haya,
tukiangalia waimbaji wetu,ndani yao lipo kundi kubwa lililochangamana nao,maana kile wakiimbacho wale waliochangamana hakina UVUVIO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.
Ngoja nikupe mfano ;
Kwa wale ndugu zangu wasomi wafanyao kazi maofisini kuna kitu kinaitwa '' ATTACHMENT.''
Attachment ni kiambatanishi
Kiambatanishi hiki kinahitajika sana na huwa mara nyingine barua nyingine zile zenye ujumbe mzito ni lazima ziwe na kiambatanisho(Attachment) pasipo attachment hazipokelewi huko ziendako.
Alikadhalika waimbaji wa nyimbo za injili wanahitaji attachment/Kiambatanishi.Kiambatanishi cha waimbaji ni UWEPO WA UDHIHILISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU kwa kile wakiimbacho. Ukiona hakuna hilo basi usipate shida sana kujiuliza,ujue ndio wale miongoni mwa kundi kubwa lililochangamana. Pia hata baadhi ya watumishi mbali mbali nao ni vivyo hivyo,wapo waliochangamana.
MWISHO.
Mawasiliano yangu kwa huduma ya maombezi
ni 0655-111149.
UBARIKIWE.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni