Alhamisi, 23 Januari 2014
HIVI NI VIGUMU KUSUBIRI MPAKA NDOA? MBONA WENGINE WANAWEZA, SOMA MWENYEWE
Megan Good na mumewe Devon Franklin walisubiri mpaka ndoa.
Mariah Carey na mumewe Nick Cannon
Suala la kusubiri kuingia kwenye uhusiano wa mke na mume kabla ya ndoa limekuwa na matatizo kwa watu wengi haijalishi cheo au imani zao, kutokana na kitendo hiki watu wengi wamejikuta wakiangukia dhambini kwakuanza kuishi kama mke na mume kabla ya ndoa ama baada ya kukaa kwa muda mrefu na kujaaliwa watoto ndipo hukumbuka kurudi kanisani kubariki ndoa zao. lakini pia kuna wale ambao wanataka kujaribu na kujikuta wakipanda madhabahuni tayari wamechoka, ndoa ambazo zimeongezeka kwa kasi sana nchini.Hili linaweza kukustua moyo wako na yawezekana usiamini lakini ni kweli imetokea na imetangazwa katika baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu wasanii maarufu katika nyanja mbalimbali ambao wamekaririwa na vyombo hivyo wakisema hawajawahi kushiriki tendo la mume na mke kabla hawajaoana na wapenzi wao.
Kati ya watu hao ni pamoja na mwimbaji maarufu Mariah Carey na mumewe Nick Cannon walisubiri
mpaka wakaoana huku Mariah akikaririwa akisema walipopendana waliahidi kusubiri kushiriki kuumega mkate mpaka watakapooana na ndicho kilichotokea usiku wa ndoa yao ndipo walipoanza kushiriki kula mkate. Wengine ni mwanadada Meedan Good ambaye amelelewa katika malezi ya Kristo anasema yeye na mumewe DeVon Franklin ambaye ni mmiliki wa studio na muhubiri walisubiri kushiriki tendo hilo mpaka usiku wa ndoa yao.
Katika mwendelezo wa listi ya watu hao maarufu kama ilivyoorodheshwa na mtandao wa BREATHECAST ni pamoja na Kevin Jonas kutoka kundi la The Jonas Brothers ambao kwa pamoja walivaa pete maalumu kuonyesha kwamba watasubiri kufanya tendo hilo mpaka watakapooa na si vinginevyo. Tim Tebow ambaye ni mchezaji soka wa Kikristo maarufu nchini Marekani amekiri mbele ya waandishi wa habari kwamba anasubiri Mungu ampatie ubavu wake ndipo afanye tendo hilo.
Ukiachana na listi hiyo ndefu pia yumo mwimbaji nyota wa muziki wa injili aitwaye Rebecca St. James anafahamika kwa msimamo wake wa kusubiri mpaka ampate mwenza wake wa maisha ambaye anasema anataka ajivunie kwake kwakuwa alikuwa akimsubiri yeye kwa wakati wote huo. angalia mahojiano yake katika video hapo chini.
Hawa walisubiri. ©Reuters/instagram.
Yawezekana kuna wakati ulipita katika majaribu ambayo yalikufanya uanguke katika imani yako kutokana na mazingira yaliyokuwa yamekuzunguka, swali la kujiuliza je? baada ya kugundua kwamba umeanguka ni hatua gani ulichukua ya kuendelea kugalagala kwenye hayo matope ama uliamua kumrudia Mungu wako ingali mapema? kumbuka Mungu wetu ni mwenye rehema ambaye hutuita siku zote na hutusamehe makosa yetu na kuyafuta kabisa endapo tutatubu na kutaka toba ya kweli. Yawezekana ni kwakipindi kirefu umekuwa katika hali ya kutafuta mwenza mpaka imefika hatua ya kukata tamaa, kikubwa ninacho kushauri hebu kumbuka kuvunja maneno yote yaliyowahi kunenwa juu yako ama umewahi kujisemea wewe mwenyewe kwamba hautaolewa ama kuoa maana maneno huumba. Vunja laana zote za maneno na kutubu yote uliyotenda, kabidhi maisha yako kwa Yesu nina hakika atafanya kitu katika maisha yako. Barikiwa
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni