Jumamosi, 4 Januari 2014
TAFSIRI YA NAMBA 14 KIMAANDIKO!
Pastor Peter Mitimingi, mkurugenzi Voice of Hope Ministry(VHM)
1. Namba 14 ni namba ya Wokovu na Ukombozi (Salvation ;Deliverance)
2. Mwaka 2014 ni mwaka wa Wokovu na Kufunguliwa.
3. Kulikuwa na Vizazi 14 kutoka Abraham mpaka Daudi
4. Kulikuwa na Vizazi 14 kutoka Daudi mpaka Utumwani Babeli.
5. Kulikuwa na vizazi 14 Kutoka Utumwani Babeli hadi Kristo.
Mathayo 1:1- 17
6. Miaka 14 baada ya Yerusalem kuharibiwa Ezekiel alipata maono juu ya Hekalu jipya. Ezekiel 40.
7. Ilikuwa ni siku ya 14 Mtume Paulo na abiria wenzake kupata chakula baada ya kuwa kwenye doruba. (Matendo ya Mitume 27:27)
8. Nuhu alimtuma njiwa nje ya safina mara mbili na kusubiri kwa jumla ya siku 14 na kuleta taarifa ya maji kukauka. (Mwanzo 8:9-12)
9. Mfalme Suleiman pamoja na watu wake walikuw ana siku 14 za kusherekea Hekalu jipya. (1Wafalme 8:65)
10. Hezekia na watu wake walikuwa na siku 14 kusherekea Pasaka ambayo haikuwa imesherekewa kwa muda mrefu kwahiyo ilikuwa ni kama mwanzo mpya. 2Mambo ya nyakati 30:15…)
11. Yakobo alitumikia miaka 14 kupata wake zake na ndipo maisha yake yalianza rasmi. (Mwanzo 31:41)
12. Yusufu baada ya miaka 13 ya utumwa na gerezani mwaka wa 14 alianza kuishi maisha ya raha kama mtawala na sio mtuma na mfungwa tena.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni