Leo wakristo wengi hupenda kuongozwa na ROHO katka maamuzi yao ya kila siku,lakini hawajui namna ROHO amuongozavyo mtu
Biblia inatuonyesha njia kadhaa ambazo Roho wa Mungu huzitumia kuwaongoza watu wake.Pindi unapotaka kufanya jambo utasikia ndani yako uhuru au kufunguka, hii ni moja ya njia anayotumia Mungu kumuongoza mtu wake.Ikiwa unataka kufanya jambo kasha ukasikia uzito,mashaka au ugumu ndani yako hakuna hali ya kufunguka ndani juu ya hilo ujue hauko sahihi rudi na jipange upya katika Kristo.kwa nini iwe hivi? “Kwa kua hamkupokea roho ya utumwa iletayo hofu…Warumi8;15”,hivyo ile hali ya hofu,ugumu,na kutokufunguka ndani pindi unapotaka kufaya au ufanyapo maamuzi fulani ni ishara kua MUNGU yuko mbali na hilo jambo. lakini “mkiongozwa na Roho hamko chini ya sheriaGalatia 5:18”. Hampo chini ya sheria maana yake hamfanyi lolote kwa kulazimishwa ila kwa upendo wa kristo ulio ndani yetu unaotufanya tuwe huru kufanya bila hofu kwa kua kiini cha maaamuzi yetu ni Roho akaaye ndani yetu na sio utashi wetu wenye lengo la kutimiza tamaa za mwili

Upendo wa MUNGU kwetu ni mkuu (Great), na upo kutuongoza pindi tunapotafuta msada kwa MUNGU juu ya maamuzi yetu ya kila siku.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni