Jumatatu, 20 Januari 2014

NYOTA WA MUZIKI WA INJILI MAREKANI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI


Mwimbaji anayetamba na limbo wake maarufu "Breaks every chains" Tasha Cobbs wa nchini Marekani amefiwa na baba yake mzazi askofu Fritz Cobbs katika taarifa ambayo ilitolewa na mwimbaji mwingine wa injili nchini humo James Fortune kupitia mitandao ya kijamii kwakuwataka wapenzi wa muziki wa injili kumkumbuka katika maombi mwimbaji huyo kwakuwa amefiwa na baba yake mzazi.

Aidha kwa upande wake Tasha hakuandika chochote kuhusu msiba huo isipokuwa amewashukuru mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kwa maombi yao na kumalizia kwakuwaambia kwamba anawapenda.




Tasha Cobbs
16 hours ago
Hey Family! Thank you for your thoughts and prayers! They are felt! Love you guys!
Tasha Cobbs ambaye siku za hivi karibuni alijinyakulia tuzo za Stellar awards katika kipengele cha mwimbaji mpya wa mwaka kupitia album yake iliyotengenezwa na mwimbaji na mwandaaji wa muziki VaShawn Mitchell ikiwa na wimbo maarufu wa "Break Every Chain"

Mwimbaji huyo alikuwa jijini London pamoja na mwimbaji mwingine Micah Stampley na kundi lake wakati wa sikukuu za mwaka mpya chini ya mwaliko wa kanisa la Ruach Ministry lililochini ya askofu John Francis lililopo Kilburn ambaye amekuwa akiwaalika waimbaji tofauti wa injili kila mwaka kutokea nchini Marekani.

Mapema mwaka jana gwiji wa muziki wa injili nchini humo Donnie McClurkin alifiwa na wazazi wake wote wawili lakini pia wakati mwaka mpya ukianza gwiji huyo alijikuta kipindi chake cha radio kikiondolewa na wamiliki wa radio ya WBLS/WLIB na nafasi yake akapewa askofu Hezekiah Walker na kuwataka mashabiki waliokuwa wakisikiliza kipindi chake kumpa sapoti askofu huyo ambaye aliteuliwa na radio kuchukua nafasi yake, ombi ambalo hata hivyo mashabiki ndugu, jamaa na marafiki wa mwimbaji huyo asilimia kubwa wameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho na wengine kuahidi kutosikiliza.



Nikiwa na James Fortune mwimbaji aliyetoa taarifa za kifo cha baba yake Tasha, hapa ilikuwa Ruach Ministry Kilburn jijini London mwezi January 2013.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni