Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Amina Salum (Chini katika picha) ambaye hapo awali kabla ya kuokoka alikuwa muislamu, alikuja katika mkutano wa Ufufuo na Uzima akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali.
Akieelezea tatizo lake, Amina alisema kuwa alikuwa na tatizo la tumbo ambalo alikuwa akisikia kuwa tumbo linachoma choma ndani kiasi cha kushindwa kula. Tatizo ambalo lilimdhoofisha mwili siku hadi siku.
Wakati Mchungaji Gwajima akipita katikati ya makutano alimkuta amekaa na mapepo yaliyokuwa ndani yake walipomuona mchungaji wakadhihirika kutokea ndani yake ambapo na baadaye yalipewa amri yamtoke mtu huyo. Baada ya hapo dada huyo alipona kabisa magonjwa yake papo hapo.
Mchungaji Gwajima akiwa amemshika Amina baada ya kupokea uponyaji wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni