Jumapili, 5 Januari 2014

IBADA YA MWAKA MPYA NA CHAKULA CHA BWANA LUTHERAN LONDON



Hapo jana katika kanisa la Kilutheri usharika wa mtakatifu Anne's jijini London kumefanyika ibada ya kiswahili ya jumapili ya kwanza ya mwezi kama ilivyoada ikiongozwa na mchungaji kiongozi Tumaini Shekhalage akisaidiwa na mchungaji Moses.

Ibada hiyo ya mwaka iliyopambwa na waimbaji wa Furaha kwaya ama kwaya kuu iliambatana na ibada ya chakula cha Bwana pamoja na neno la Mungu lililohuburiwa na mchungaji Tumaini aliyewakumbusha waumini waliohudhuria kanisani hapo kukumbuka kusamehe na kuachilia ili wapate kuendelea katika mambo yao kwakuwa chuki si nzuri ni kikwazo cha maendeleo lakini pia ni dhambi kwa Mungu.

Aidha mchungaji Tumaini aliwataka watu kukumbuka kushikilia vyema nafasi walizopewa ili waendelee kuishi kwa amani na maendeleo, akiwataka wenye ndoa kulinda ndoa zao, maboss makazini kulinda nafasi zao na sio kuzipoteza kwa makatibu mukhatasi wao pindi wanaporuhusu mambo mengine kufanyika na kujikuta heshima ya ubosi kupotea. Katika ibada hiyo pia mchungaji Tumaini aliwatambulisha watoto watakaoanza darasa la kipaimara kwa mwaka huu pamoja na kuwepo kwa ibada ya kumsimika askofu mkuu wa lutheran Uingereza itakayofanyika mji wa Liverpool nchini humo.

Ibada nyingine ya kiswahili inatarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu kuanzia saa nane mchana.



Mchungaji Tumaini akihubiri.




Baadhi ya waumini wakisikiliza ujumbe wa neno la Mungu.




Furaha kwaya wakimtukuza Mungu.




Mchungaji Moses akishirikiana na Mchungaji kiongozi Tumaini Shekalage kuongoza ibada ya chakula cha Bwana.




Waumini wakipanga mstari kwenda kupokea chakula cha Bwana.





Vijana wa darasa la kipaimara wakiombewa na mchungaji Moses


Vijana wa darasa la kipaimara wakiwatazama washarika.


Waumini wakipata chai na vitafunwa baada ya ibada.


Wadau wakubwa wa Gospel Kitaa bwana Andy Kilo Mkwavi mkono wa kuume na rafiki yake wakipozi mbele ya kamera ya GK.


Chai na vitafunwa.


Mchungaji Moses akizungumza na muumini wake Sakina Mwamwaja huku wakipata chai.


Tukifurahia jambo na big dada Sakina na rafiki yetu. Karibu tarehe 19 saa nane mchana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni