
Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe....
Haleluya....
Kupitia Biblia maandiko matakatifu,wapo Lazaro wawili tuwasomao.
Lazaro wa kwanza ni yule aliyekuwa muombaji,mtu aliyekuwa akiwekwa mlangoni mwa tajiri mmoja,akishibishwa kwa makombo,mtu aliyekuwa maskini. (Luka 16:19-31).
Lazaro wa pili ndio yule ambaye alikuwa hawezi na baadaye akafa. Huyu alikuwa ni mkazi wa Bethania,mwenyeji wa mji wa Mariamu.Lazaro huyu alikuwa pia mfuasi wa Kristo Yesu,pia alikuwa rafiki wa Bwana Yesu Kristo.Kupitia habari za Lazaro huyu wa pili,ndio nataka tujifunze kidogo.
Wengi wetu tulishasoma habari zake Lazaro kipitia kitabu cha Yoh.11:1-44
Lakini si wote wenye kuelewa fundisho la Lazaro.
Lakini leo ipo Neema ya pekee mahali hapa ya kujifunza zaidi kwa habari hii.
Yapo mengi ya kujifunza kupitia habari ya Lazaro,nasi tutajifunza kwa kadri ya Roho apendavyo.
Biblia inatuambia yakwamba Lazaro alikuwa mkazi wa Bethania,ambapo neno
BETH ni neno lenye asiri ya kiebrania lenye maana NYUMBA(House)
Pia na neno,
..ANIA.. Ni neno lenye asiri ya kiebrania lenye maana YA KIMASKINI (of poor)
Hivyo ukiyaunganisha maneno haya,utapata hivi;
BETHANIA=Nyumba ya kimaskini(the house of poor)
Au ukanda wa kimaskini.