Jumamosi, 28 Septemba 2013

VIONGOZI WA KIDINI KENYA KUONGOZA MAOMBI YA KITAIFA JUMANNE


Rais Uhuru Kenyatta na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la mpwa wao marehemu Mbugua Mwangi na mchumba wake Rosemary Wahito ambao waliuawa katika tukio hilo la kigaidi. Picha na Daily Nation Kenya.
Viongozi wa kidini nchini Kenya wanatarajia kufanya maombi kwa taifa lao siku ya jumanne ijayo katika viwanja vya KICC kuanzia majira ya saa nne asubuhi. Akitoa tangazo hilo katibu mkuu wa taasisi ya jumuiya ya Kikristo nchini humo National Christian Council of Kenya (NCCK) bwana Peter Laranja amewataka watu kutoka madhehebu yote pamoja na viongozi wa dini zote kukutana hapo kwa ajili ya kuiombea Kenya.www.gosplekitaa.blogspot.com

Laranja amewataka wakenya kuonyesha umoja na nguvu kwa pamoja licha ya hayo ambayo yametokea katika jengo la biashara la Wastegate ambalo watu zaidi ya 60 wameripotiwa kufariki dunia wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya baada ya watu zaidi ya 10 ambao inaaminika ni wanachama wa kundi la kigaidi la Al Shabaab kuvamia jengo hilo mchana wa jumamosi iliyopita.

Aidha pia viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo aliyekuwa waizir mkuu wa kwanza wa nchi hiyo cheo ambacho hakipo tena kwa wakati huu mheshimiwa Raila Odinga amekaririwa akisema kuwa magaidi wasiwagawe wakenya bali waendelee kuonyesha umoja wao na kumalizia kwakusema kwamba fikra na maombi yake yafike kwa familia zote zilizopoteza ndugu zao katika tukio hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni