Jumatatu, 30 Septemba 2013

ONAJINSI WALIOCHUKULIWA MSUKULE WALIVYO RUDI KWA MAOMBI ARUSHAM NA Mchungaji Gwajima

MWANAMKE ALIYEKUFA MIAKA MINGI ARUDI MKUTANONI ARUSHA WATOTO WAKE WAZIMIA BAADA YA KUMTAMBUA

Mama wa kwanza kushoto anayedaiwa kufariki siku nyingi akiwa mkutanoni na mwanamke mwingine ambaye pia alichukuliwa msukule, hapa ni baada ya kuanguka karibu na eneo la mkutano, kumbe watoto wake walikuwa mkutanoni pia.www.mwakasegebibilia.blogspot.com



Mmoja wa mabinti aliyezimia baada ya kumuona mama yake aliyefariki dunia siku nyingi.



Mchungaji Mwangasa akajaribu kuwatuliza watu kuwa muda wa kibali cha mkutano ulikuwa umeisha ndipo likaibuka lingine baada ya kuwahoji watu hao.

Kumbe, walianguka kutoka hewani ghafla eneo la mkutano, jambo lililowashtua wengi na kuhusu moja kwa moja kuwa ni wachawi. Katikati ya mawazo hayo wakajitokeza mabinti watatu na kusema kuwa yule mwanamke mzee ni mama yao aliyekufa miaka mingi iliyopita. Na mara baada ya kusema hivyo wote wakazimia hapo hapo. Na kuleta kizaazaa kingine.

Umati wa watu ulirindima kwa kelele na fujo na kwa giza hilo ikaonekana si vyema kuendelea na mkutano ndipo ulipoahirishwa na watu kurejea makwao wakitazamia jioni ya leo kusikia ushuhuda kamili.







Mwanaume aliyerudishwa msukule baada ya maombi yaliyofanywa na mchungaji Gwajima kushoto.



Mchungaji Gwajima akiongoza maombi kwa maelfu ya watu waliofika mkutanoni hapo, Arusha kwa Yesu.


Endelea kuungana nasi ili kupata kilichojiri baada ya hapo... ama tembelea page ya kanisa la Ufufuo na Uzima



MUNGU KWETU SISI NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE

Maoni 1 :

  1. Mungu ni muweza yote,hakika ataitwa Mungu siku kwa siku !

    JibuFuta