Kati ya siku ambayo wakazi wa Arusha walipata kufunguliwa dhidi ya vifungo vilivyokuwa vinawasumbua, basi ni siku ya Jumapili ambapo mkutano mkubwa ulioandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima umefikia siku ya tatu.
Wakazi hao walioanza kufurika kwenye viwanja vya reli kutoka kona mbalimbali ya mji huo, hatimaye walipata chakula cha kiroho na kufunguliwa kwa mamlaka ya Jina la Yesu. Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio la mkutano huo ambao Gospel Kitaa ilipata fursa ya kuwepo na kushuhudia namna ambavyo Mungu anatumia watu wake kuponya wenye shida na matatizo
Siku ya 4 ya mkutano Mchungaji Gwajima atahubiri kuhusu aina za misukule. Usikose kuhudhuria kwani mwisho wa mkutano huu wa wiki mbili, utapata uwezo wa kutambua aliyefariki na aliyechukuliwa kwa njia za ajabu.
|
Mchungaji Gwajima akihubiria maelfu ya wakazi wa Arusha na waliojitokeza kumpoke Yesu kuwa mwokozi wa maisha yao. |
|
Mara baada ya kuongozwa sala ya toba, wakarejea kwenye viti vya, ambapo walitakiwa kuendelea kupata huduma kwenye kanisa lolote la kiroho linalomhubiri yesu na kunena kwa lugha. |
|
Moto miguuni, mwanadada akifunguliwa dhidi ya vifungo |
|
Kijana anayeteswa na mapepo akikimbizwa ili hatimaye uponyaji umfikie baada ya maombi.
|
|
Mchungaji Gwajima akisifu pamoja na Mwanamapinduzi jukwaani. "Saa ya Ufufuo na Uzima" |
|
Mwanamapinduzi akimsifu Mungu pamoja na wananchi uwanjani. |
|
Sehemu ya watenda kazi na watu waliofunguliwa na huduma ya ufufuo na uzima wakiwa karibu na jukwaa. |
|
Ofisi za habari za huduma ya ufufo na uzima ambapo DVD na vitabu vinapatikana. |
|
Mtaalamu wa uezezi wa habari wa huduma ya ufufuo na uzima, Davie Abson akiwa kazini |
|
Wadau wa Gospel Kitaa |
|
Mdau mmojawapo wa Gospel Kitaa, Baraka, ambaye alibahatika kupata picha na mwanaGK, Elie. |
|
Taswira ya viti baada ya watu kurejea makwao siku ya tatu ya mkutano huo. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni