Ijumaa, 27 Septemba 2013

HARUSI KTK BWANA NI SIMON NA ASIGELE SONELO .



Shangwe za GK hii leo tunakwenda kwa mmoja wa waimbaji katika moja ya kwaya zinazofanya vyema sana katika tasnia ya uimbaji jijini Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla bwana Simon na mkewe Asigele Sonelo ambaye ni mwanakwaya wa Efatha ya Uhuru Moravian Kariakoo au waite wana wa "Twaomba Amani" au wana wa "Usalama", wapenzi hawa wawili walifunga ndoa yao iliyofana sana katika kanisa la Moravian Uhuru Kariakoo jijini Dar es salaam na kufuatiwa na sherehe kubwa ya kuwapongeza iliyonogeshwa na waimbaji wenzake wa Efatha pamoja na mwanamama Bahati Bukuku. Angalia baadhi ya picha mambo yalivyokuwa.


Matron mrs Nsajigwa au mwite Tupilike mama Victorio akipambwa.www.mwakasegebibilia.blogspot.com
Vazi rasmi la bwana harusi likisubiria kuvaliwa. 

Bwana Nsajigwa Richard akimweka sawa bwana harusi.


Asigele akijiweka sawa.


Akiwa ameshamaliza salon, tayari kuelekea church.
Mchungaji akiendesha ibada.
Efatha Uhuru Moravian wakienda sawa.

Efatha wakiimba kwa furaha.
Viapo vikaanza.
Na pete zikavishwa, ndaga fijo mwe!

Da! namimi kidole kinang'aa sasa rahaaaaa.










































Mungu awabariki sana katika ndoa yenu, awape uvumilivu, kupendana, kuwezeshana na kufanikiwa sana kimwili na kiroho. Amen

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni