Ijumaa, 27 Septemba 2013

pigo,,MPIGA BASS NYOTA WA JOYOUS CELEBRATION ANUSURIKA KIFO


www.mwakasegebibilia.blogspot.com
Sabelo katika picha baada ya ajali.
Ikiwa siku ya jana na leo kundi la Joyous Celebration linafanya onyesho lake la nyimbo za zamani kwa kualika waimbaji waliowahi kuimba na kundi hilo, mmoja kati ya wapigaji mahiri waliowahi kutumika katika kundi hilo wakiwajibika katika gitaa la bass mwanakaka Sabelo Masondo amenusurika katika ajali mbaya ya gari alilokuwa akiliendesha.

Masondo ambaye ameachana na kundi la Joyous zaidi ya miaka mitatu sasa amepata ajali hiyo mbaya kwa gari alilokuwa akiliendesha aina ya pick up kupinduka zaidi ya mara sita nayeye akitoka na majeraha madogo ikiwemo kuumia sehemu ya jicho huku gari likiwa katika hali mbaya, katika ujumbe wake alioutoa katika ukurasa wake wa Facebook nyota huyo wa kuliungurumisha gitaa zito amemponda shetani kwakuimba wimbo maarufu uitwao "How great is our God" na kumwambia shetani kwamba Mungu ni mkuu na kwamba hatoweza kamwe kumsogelea ama kujilinganisha naye, na kwamba yeye Sabelo anasonga mbele daima.

Nyota huyo akamalizia ujumbe wake kwakusema yeye ni mzima kabisa na amemshukuru Roho Mtakatifu kwakumkumbusha kuomba asubuhi kabla hajatoka nyumbani kwani ndiko kumeokoa maisha yake na kumalizia kwakusema hakuna rafiki kama yeye kwani hata vidole vyake viko salama na kuachia kicheko cha ushindi.

Sabelo amepigia kundi la Joyous Celebration kwa mafanikio makubwa kutoka album ya 11 hadi ya 14 kisha kuendelea na makundi mengine ambayo amekuwa akiyapigia kwa mikataba ambapo aliyebeba mikoba yake ndani ya Joyous ni mwanakaka Bheka Mthethwa. Wakati huohuo waimbaji mbalimbali wa zamani wa kundi hilo wamependezesha usikuwa MTN Joyous Celebration rewind ambayo inafanyika katika ukumbi wa Teatro Montecasino ambapo mmoja kati ya waimbaji hao ni mwanadada mrembo Hlengiwe Dlamini Pitso ambaye alitamba na kibao cha Nkosi yamile katika album ya 12 ya kundi hilo.

Sabelo enzi zake na Joyous hapa ni katika toleo la 13.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni