Jumatatu, 30 Septemba 2013

ASKOFU SOLLO AMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA KUENDESHA NCHI KWA AMANI




HUKU nchini kenya hofu ya vitendo vya ugaidi vilivyofanywa na watu wanaosadikika kuwa kundi la wanamgambo wa al-Shabaab katika eneo la maduka ya bidhaa la Westgate mjini Nairobi ikiendelea kutawala nchini Kenya, askofu wa kanisa la maombezi na uponyaji cha Overcomers (OPC) mkoani Iringa Dr Boaz Sollo amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuendelea kuliongoza Taifa katika hali ya amani na utulivu na kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini kote nchini kujikita katika maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania amani ili yaliyotokea Kenya yasiikumbe Tanzaniawww.mwakasegebibilia.blogspot.com


Askofu Dr Sollo alitoa kauli hiyo jana katika ibada yake ya kwanza baada ya kupokelewa na waumini wake akitokea nchini Marekani kwa huduma ya maombezi kwa Taifa la Marekani .

Alisema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi za mfano barani Afrika kwa kuwa na amani kutokana na uwajibikaji na utendaji mzuri wa Rais Kikwete na watendaji wake wote na kuwa ili yale yaliyotokea nchini Kenya kwa watu kuvamiwa na kudi hilo la kigaidi la Al-shabaab ni vema sasa viongozi wote wa madhehemu ya dini kuelekeza nguvu zao zote za kimaombi katika ibada maalum za kuliombea Taifa amani .

Kwani alisema kuwa silaha kubwa katika kupambana na adui awaye yoyote ni maombi na kuwa siku zote Mungu husimama katikati ya wanamaombi na kamwe shetani hafungamani na Taifa lolote ambalo watu wake watakuwa ni wacha Mungu .

" Awali ya yote naungana na watanzania wote pamoja na viongozi wa serikali yetu tukufu katika kuwafariji ndugu zetu na jirani zetu wa Kenya ambao ndugu zao wamepoteza maisha katika shambulio baya lililotokea hivi karibuni katika eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi....Mungu aendelee kuwapa roho za uvumilivu ....ila pia kwetu viongozi wa dini nchini Tanzania tunawajibu wa kutenga muda wa kuliombea Taifa letu amani "alisema askofu Dr Sollo

Kuwa kanisa lake la OPC limejipanga kuendeleza maombi ya kuliombea Taifa na kuwa hadi sasa jamii ya wana Iringa kwa ujumla kutokana na kazi kubwa inayofanywa na kanisa hilo hata matukio ya ajabu ajabu ambayo yalikuwa yakitokea kutokana na watu kuanguka katika dhambi yameanza kutoweka.

Wakati huo huo askofu Dr Sollo alitaka viongozi wa dini kuendelea kuuombea mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili umalizike salama na kuwa Taifa moja kama ambavyo lilivyosasa pia kuiombea katiba kuendelea kutoa uhuru wa kuabudu pamoja na kutowanyima uhuru watu wake hasa viongozi wa dini kukemea vitendo vya ushoga kama ilivyo nchini Marekani ambapo wahubiri wamezuiwa kabisa kugusia wala kuzungumzia kwa maana ya kupinga suala la ushoga katika nyumba za ibada.

" kabla ya kuanza kufanya shughuli zangu za mahubiri nchini Marekani wenyeji wangu waliniweka sawa na kunieleza kuwa sipaswi kuzungumzia suala la ushoga katika mahubiri yangu na nikifanya hivyo nitafukuzwa nchini humo.....ila sisi huku Tanzania serikali haitupangii mambo ya kuzungumza bora mradi hatuzungumzii kauli za kichochezi"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni