Jumamosi, 21 Septemba 2013

Historia ya Mwanamuziki Donnie Mcclurckin


Pastor Donnie Mcclurkin

Donnie Mc Clurkin ni Mwanamuziki Mashuhuri wa nyimbo za Injili na Mchungaji wa Kanisa la Perfecting Faith church lililo katika jimbo la Detroit nchini Marekani.


Donnie alizaliwa na Familia ya Bw Donald Sr na Mama Frances Mcclurkin mnamo Jan 25 mwaka 1959 na kukulia katika mji wa Louisville. Akiwa na umri wa miaka nane(8), mdogo wake wa kiume mwenye miaka miwili(2) aligongwa na gari na kufa papo hapo huku Donnie akishuhudia.Wakati Donne akiwa na majonzi mazito usiku huo huo ambao walimzika mdogo wake, mjomba wake alimbaka Donne.



Baada ya kifo hicho familia yake iliingia kwenye mgogoro kubwa ambao ulitokana na utumiaji wa dawa za kulevya. Baada ya kufikisha miaka 13, binamu yake mtoto wa mjomba wake alimbaka Donnie pamoja na dada zake wawili kitendo amabacho kilimuumiza sana na kumuachiia kovu la aina yake. Muda wote alijiona mkosaji, mtu aliyekandamizwa na hakuwa na ujasiri mbele za watu na mwenye wingi wa aibu.www.mwakasegebibilia.blogsspot.com

Kwa kipindi hicho chote alipata Faraja toka kwa shangazi yake ambaye alikuwa muimbaji wa nyimbo za Injili. Shangazi yake huyo alimfanya Donnie ajiingize kanisani na kuanza kupiga piano na kuimba kwaya kama sehemu ya kufuta machungu na kuondokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao. Mama yake mzazi naye alikuwa muimbaji kanisani hivyo kanisani kukawa ndio nyumbani kwake na kambi yake pindi nyumbani kukitokea matatizo.


Tarehe 14 Julai 1969 akiwa na miaka takribani kumi(10) ikiwa ni siku ya jumapili akiwa kanisani huko Amityville Gospel Tabernacle mtumishi wa Mungu aliyekuwa akihubiri aliwaambia watu kuwa “KRISTO ALIKUFA KWA SABABU ANAKUPENDA” wazo hili hilo ndilo lilikuwa kwa Mcclurkin ndipo akaamua kuyakabidhi maisha yake kwa Yesu. Kwenye kitabu alichoandika kuhusu maisha yake alisema “ Kanisa limekuwa ndio ulimwengu wangu mahali ambapo najisikia Amani na najisikia kama ndio Mahali Pangu halisi”







Mwaka 1971 wakati anamiaka 11, alikuwa akimpenda sana mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili kipindi hicho aliyeitwa Anre Crouch. Siku aliposikia kua Crouch anakuja katika jimbo lao alimuomba mama yake ruhusa waende kwenye tamasha na kumuahidi jumatatu yake ataamka mapema na kwenda shule kama kawaida. Mama yake alikubali na wakaenda Tamashani na Donnie akaenda kukaa mbele kabisa sambamba na mamaye.
Baada ya Crouch kuingia ukumbini saa tano usiku kabla hajaanza kuimba alimuona Donnie na kumfata, Donnie anasema, Crouch akaniuliza kitu gain unafanya hapa, nkamjibu nakusubiri wewe!!, akaniuliza kama nimelipenda Tamasha nkamjibu ndio, akanambia wakati yuko mdogo hakuweza kuimba wala kucheza mpaka baba yake alipomuobea. Nkamjibu baba yangu hajaokoka hivyo hawezi kuniombea. Mwishoni akaniuliza kama nitapenda aniombee nami nkamkubalia. Akaweka mkono wake kichwani kwangu akasema“Mungu mpe kile ambacho umenipa mimi” kisha akaelekea stejini. Huo ulikuwa ndio mwanzo wa hiki nlichonacho leo.

Akiwa kanisani hapo alianzisha kundi llilokuwa linajulikana kama The Mcclurkin Singers na baadaye alianzisha kundi lililokuwa likijulikana kama The New York Restoration Choir. Mwaka 1983 wakati akiendelea kutumika na kwaya alikutana na Pastor Marvin Winans. Mch Winans alivutiwa sana na namna Donnie alivyokuwa akiimba kwenye semina ya injili.


Baadaye Mch Winans alimwalika Mcclurkin katika mji wa Detroit alikokua akiishi ili kumsaidia kuanzisha huduma(kanisa) liitwalo Perfecting Faith Church.Miaka sita baadaye(1989) Donnie aliamua kuhamia Detroit na kuanza kufanya kazi na Pastor Winans. Katika kipindi hiki ndipo Mcclurkin alipata wasaa wa kuzunguka sehemu mbalimbali na kufanya huduma akiwa chini ya pastor Winans. Donnie anasema Familia ya Winans imekuwa karibu sana nay eye Kuanzia Bebe, Cece, na Pastor Marvin na wakat mwingine anafkiri yeye ni Donnie Mcclurkin Winans.



Donnie Mcclurkin na Cece Winans wakiwa wameshikilia tuzo za Trumpert awards walizopewa mwaka 2007

Mwaka 1991 alikuwa hajiskii vizuri kiafya, hivyo alienda Hospitali, walipompima walimwambia kuwa anaugonjwa wa Leukemia(kansa ya damu), na madaktari wakamwambia unahitaji matibabu ya haraka. Akawambia naombeni mnipe siku 60 ili nkaongee na Baba yangu(Mungu). Nkawasiliana na Pastor Andre Crouch naye akamshirikisha baba yake ambaye kwa muda huo alikuwa Askofu jijini Califonia. Wakaomba nami nkaomba Leukemia ikaondoka, madaktari waliponipima tena hawakuikuta tena kansa mpaka leo Kristo amenipomya anasema Donnie.


Akiwa na Pastor Winans, alisaini mkataba na kurekodi album yake iliyoitwa LP, Album hiyo iliyokuwa na nyimbo kama Stand iliyongoza kwa umaarufu na kuzinduliwa na Oprah Winfrey. Nyimbo hii ilitunukiwa tuzo ya Grammy kwa mwaka huo wa 1996 kwa upande wa nyimbo za Injili. Album z\ake tatu za solo zilikamata nafasi za juu sana kwenye chati za Bilboard.


Akiwa na furaha ya ajabu Mcclurkin kupitia makongamano mbalimbali huwasimulia watu ukweli wa maisha yake huku akipinga kwa nguvu mahusiano ya jinsia moja. Mcclurkin anaamini kwamba suala la Homosexuality ni suala la kiroho haliwezi tibika kisaikolojia na linahitaji msaada wa Mungu pekee. Baada ya watu wengi kuwa wanamuomba aelezee historia ya maisha yake, Mcclurkin aliamua kurudi nyumbani kwao Amityville New York na kumuomba Mama yake ruhusa ili aandike kitabu kuhusu maisha yake.





Frances Mcclurkin (mamaye), alimruhusu Donnie aandike kitabu kinachoyaelezea maisha yake kinaga ubaga, ndipo Mcclurkin akatumia miezi 18 kuandika kitabu hicho ambacho alikiita ETERNAL VICTIM, EXTERNAL VICTOR. Alisema aliamua kuandika kitabu sio kwa kusudi la kuweka wazi uovu uliokuwa ukifanyika ndani ya Familia yao bali kwa sababu yeye ni Mwalimu, na mwalimu ni vizuri ajitoe yeye kama ujumbe ili watu wengine wajue kuwa hawako peke yao kwenye mambo wanayopitia.


Mwaka 2008 Mcclurkin alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanamuziki ambao watakuwa kwenye timu ya Barak Obama katika harakati za uchaguzi wa nchini Marekani. Mcclurkin alikubali na kujumuika na Barak Obama, lakini kutokana na msimamo wake wa kupinga mahusiano ya jinsia moja, Mashoga wengi walipinga kuwepo kwake kwenye timu ya Obama. Hivyo ili kupata kura za mashoga ilibidi Mcclurkin atolewe kwenye orodha hiyo ingawa alifanikiwa kuimba kwenye moja ya kampeni za Rais Obama.



Mcclurkin, Nofle pamoja na Mary Mary wakiwa na Rais G. Bush



Tukutane jumanne ijayo ili uone tumekuandalia nini cha kukujenga kupitia maisha na changamoto za watumishi wa Mungu mbalimbali wanazo kutana nazo katika maisha .

You might also like:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni