Jumapili, 8 Septemba 2013

T.D JAKES AOMBEWA NA MUIGIZAJI TYLER PERRY, ROHO ATAWALA


Muigizaji, Tyler Perry akimnenea baraka Askofu T.D Jakes wa the Potter's House. ©Facebook/TD Jakes Ministries
Pata picha siku Masanja Mkandamizaji anamuwekea mkono Mwalimu Christopher Mwakasege na kumuombea, hakika wengi watashangaa na kudhani labda ni utani. Lakini la hasha, Mungu hutumia chombo chochote, hivi ndivyo ilivyokuwa Potter's House, kwenye huduma ya T.D Jakes, ambapo muandaaji (producer) na msanii muigizaji maarufu nchini Marekani na duniani kwa ujumla, Tyler Perry - alipomuwekea mkono Askofu T.D Jakes.www.blogspot.com

Tukio hilo limetokea mwanzoni wa wiki iliyopita ambapo hudu aya vijana likuwa inaanzishwa kanisani hapo, na ndipo Tyler alipokaribishwa kutoa mchango wake. Hapo awali Tyler alifikiria kutoa dola laki moja kumi na tatu elfu, lakini alipopanda jukwaani, Mungu alizungumza nae kwa namna nyingine, na ndipo alipoamua kutoa dola milioni moja, sawa na takriban bilioni moja za Kitanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni