Jumatatu, 16 Septemba 2013

ANGALIA INJILI NDANI YA JIJI LA KAMPALA UGANDA

www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Angalia kutoka mitaa ya jiji la Kampala nchini Uganda ambako GK ilipita na kufanikiwa kuingia katika moja ya makanisa maarufu nchini humo liitwalo Watoto ambalo makao makuu yake yanapatikana jijini hapo katika barabara ya Kampala huku kanisa hilo likifungua matawi zaidi mikoa ya nchi hiyo. Kanisa hili ndio nyumbani kwa kwaya maarufu duniani ya Watoto Children Choir, utaratibu wao wa ibada na uimbaji wao unalingana na ule wa kanisa la Hillsong ambalo pia hutoa misaada kwa kanisa hilo lililoanzishwa na Gary Skinner ambaye wazazi wake walikuwa wamisionary huko nchini Zimbabwe.

Pamoja na picha kutoka katika ibada hiyo katika kanisa la Watoto GK pia ilipita mitaani na kuona wainjilisti wengi wakujitolea wakipiga gombo lakini kamera ikafanikiwa kuwanasa wawili tu mmoja akiwa mitaa ya jinja road na mwanadada yeye alikuwa maeneo ya Entebbe akipiga injili, wote kwa pamoja walikuwa wakitumia lugha yao ya kiganda.








Hayo ndiyo makao makuu ya Watoto Church ndani ya Kampala Road nchini Uganda.












Mwinjilisti niliyetambulishwa kwa jina moja la George akipiga injili barabara ya Kampala jijini humo.



Lazima kieleweke watu wamjue Mungu, dada akipiga injili mitaa ya Entebbe Road nchini Uganda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni