Ijumaa, 13 Septemba 2013
PADRI Anselmo AMWAGIWA 'TINDIKALI' ZANZIBAR
Padri Anselmo Mwang'amba baada ya tukio la kumwagiwa tindikali.
Taarifa ambazo Gospel Kitaa imezipata kwa ufafanuzi ni kuwa Padri wa kanisa katoliki visiwani Zanzibar amemwagiwa maji yanayodhaniwa kuwa ni tindikali.
Kwa mujibu wa WAPO Radio FM kupitia kipindi chake cha Yaliyotokea jioni hii, Padri Anselmo Joseph Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, mkoa wa mjini magharibi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, alikuwa internet café majira ya saa tisa alasiri maeneno ya Mlandege.
www.mwakasegebibilia.blogspot.com
Kwa mujibu wa kamanda wa Jeshi la Polisi mjini Magharibi, Mkaadanu Hassan Mkaadanu, Padri huyo alipigiwa simu, na alipokuwa akitoka nje ili kuisikiliza vema simu, hapo ndipo tukio likatokea, ambao haijajulikana kama ni mtu au kundi la watu lililofanya tukio hilo.
Taarifa za hivi sasa zinaeleza kuwa Padri Mwang'amba amelazwa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja, wodi ya Mapinduzi mpya, ambayo ni wodi maalum kwa ajili ya viongozi.
Gospel Kitaa imeelezwa kuwa Padri huyo amefanya kazi kwa muda wa zaidi ya miaka 35 huko Zanzibar, ambapo baada ya taarifa hizi kupatikana, askofu mkuu wa kanisa katoliki Zanzibar, Agustino Shao ameelezwa kujifungia kuanzia muda huo na kuendelea kuwepo hadi muda huu ambapo ripota wa WAPO Radio FM, ameeleza.
Kwa hivi sasa taharuki ni kila mahali, hakuna kinachoeleweka, wakristo wakieleza kuwa hawana pa kukimbilia kwa kuwa ni zaidi ya miezi minne kupita tangu padri Evarist Mushi auwawe kwa risasi, na bado mwenendo wa kesi haueleweki, na kwamba sasa hawajui pa kwenda. (tazama picha za maazishi yake)
Kamanda Mkaadamu amekiri kuwa tindikali ni tatizo, na amesema kuwa wanaendelea kufanya jitihada ili kila kitu kiwe wazi.
Endelea kutembelea Gospel Kitaa, nasi tutaendelea kukufahamisha kwa kadri taarifa zitakavyozidi kutufikia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni