Jumamosi, 19 Aprili 2014

SOMO: SIKUKUU YA PASAKA

Na Mchungaji Mpambichile
Kila mwaka Wakristo duniani kote wanaazimisha sikukuu ya Kufufuka Yesu Kristo. Ni tendo la ukombozi kwa mwanadamu kutoka dhambini au kwenye mateso ya shetani.

Sikukuu hii ya Pasaka;

• Ni ukumbusho kwa wana wa Israeli walipotolewa utumwani Misri na kuelekea nchi ya ahadi ya Kanaani. Mungu alimtumia Musa katika jambo hili. Alizaliwa kwa mpango maalumu ndio maana wazalisha hawakuweza kumuua pale amri ilipotolewa kutoka kwa mfalme kuwa watoto wote wa kiume wauwawe.

Ebrania 12:23–27

• Pasaka ni siku ambayo Mungu amewafuta machozi wanadamu baada ya Yesu kushinda kifo na mauti na mwanadamu kupata wokovu na ndilo tarajio kubwa kwa wamwaminio Isaya 25:8–9. Na kumnyang’anya shetani ufunguo, leo Bwana Yesu yuko hai hata milele Isaya 1:18

Sisi tunahitaji kumwendea Yesu ingawa kwenye safari ya kumwendea Yesu ina vikwazo; dhambi, mauti, hukumu Warumi 7:21. Ni vikwazo kama vile ambavyo walikutana navyo wale waliokwenda kutizama kaburi siku ya kwanza ya Juma; jiwe limevingirishwa, muhuri katika jiwe na askari Marko 16:1 – 5. Tusiwe na sababu au vikwazo vya kutoamini Yesu Kristo amefufuka kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka dhambini. Kuteswa kwake damu iliyomwagika msalabani sisi tumepona.

Unaposherehekea Pasaka tafakari makuu aliyoyafanya Yesu juu yako. Furahi shangilia kwa maana ukombozi kwa mwanadamu umepatikana na upo leo. Ni wewe kuamua tu ikiwa bado hujaamini na kukiri kuwa Bwana Yesu ni mkombozi kwako

Pasaka hii iwe mpya moyoni mwako Yesu afufuke ndani yako acha kusherehekea kwa mazoea achia moyo wakoYesu aingie ndani yako. Ebu ona uthamani alioufanya kwetu; alitemewa mate, alipigwa mijeredi, alichomwa mkuki, alivalishwa taji ya miiba kwa ajli ya dhambi zetu. Pasaka haina maana kufanya mambo uliyoyazoea ya starehe, kukutana kwenye kumbi za starehe na kufanya dhambi haina maana hiyo. Moyo wako unapokumbuka mateso ya Kristo uwe mpya kwako.

Ebu kumbuka kuwaombea wengine; wafungwa magerezani tena wengine wamefungwa bila hatia, yatima, wajane, na wote wasiojiweza. Ili ushiriki huu wa Pasaka uwe wote sote. Mungu akubariki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni