Jumapili, 20 Aprili 2014

SOMO LA PASAKA; KUJILIWA NA MUNGU,MUENDELEZO, Na Oscar Samba

Karibu tena katika mfululizo wa somo hili linalolenga kukujuza kuhusu kujiliwa na Mungu katika maisha yetu na leo tupo katika sehemu ya pili na ya mwisho ya makala hii langu jina ni Oscar Samba tafadhali ungana nasi sasa ;yaani mimi na ROHO MTAKATIFU; Amina.
Lakini kabla ya kuendele naguswa kukujuza hili,”kumbuka Mungu anapoweka mteule wake yani kiongozi analokusudi kwako; kwa hiyo hakikisha ya kwamba unafanya kazi sanjari na mtu huyu pili kumbuka ya kwamba uongozi wa MUNGU hutoka kwa MUNGU kwa ajili ya kazi yake,fanya hivyo ukifahamu ya kuwa;
MUNGU NDIYE  ANAETEUWA NA KUCHAGUA PILI MUNGU NDIE ANAEWEKA MAONO YAKE NDANI YAKE (MBEBA MAONO) hakikisha unatembea na maono ambayo MUNGU ameweka ndani yake.
Sasa tuendele na somo letu:
YAKUPASAYO ILIUTEMBELEWE/ILI USIKOSE MAJIRA YA KUTEMBELEWA NA BWANA.
Kumbuka MUNGU hutembelea ili awe na ushirika na sisi kwa hiyo jiandae kupata nguvu za kipekee za MUNGU.Matendo ya Mitume 3  soma zaidi hapo.
Ukisoma kitabu cha Ufunuuo utaona jinsi ambvyo Yohana anakutana na Yesu akiwa katika hali ya tofauti,Kumbuka Yohana alikuwa na ukaribu sana na Yesu hata wakati wakukaribia kifo chake pale mezani Yohana alikuwa ameketi kifuani mwake.Ufunuo 1:7 na kuendelea utaona wakati ambao MUNGU alimpa ufunuo wa Yesu mfufuka,nae alipomwangalia alianguka chini kama mfu,anasema ilikuwa ni sauti kama ya maji mengi kama baragumu,nyele zake zilikuwa nyeupe maneno yake ni kama upanga.
Huo ndio uliokuwa utukufu ulinong’a kama theluji katika vazi na uso kama jua huku miguu yake ikiwa kama shaba liiyosuguliwa.Matendo 2:1 tunaona kushuka kwa ROHO MTAKATIFU aliyeshuka na kufungua mlango wa kuingia katika patakatifu patakatifu ambapo unadhiirisha ya kwamba wakati wakutembelewa na MUNGU au kujiliwa kwetu ni wakati wowote.
Wapo watu ammbao kama wewe hauta wambia ya kwamba YESU anaokoa wataenda jehenamu kwani uokovu wao unakutegemea wewe,kama Yule kiwete katika kipindi cha Pentekoste amabapo wakina Petro walimombea,kumbuka katika hekalu hili Yesu alikuwa akipita mara kwa mara ila hakumuombea.
Ukisoma katika matendo ya Mitume 3:17 na kuendelea utaona jinsi ambavyo kunasemwa nyakati au zama hizi kwa undani zaidi;
1.kuburudishwa.
2.Zama za kufanywa upya (Urejesho) na urejesho huu ni matokeo ya kutembelewa na MUNGU,hapa nachukuwa kanuni 3 za msingi zinavyoonesha jinsi ya kuingia
1.Luka 19 KANUNI YA ZAKAYO,tunajifunza kuwa na shahuku na hamu ya mambo ya MUNGU Zakayo alikuwa na shahuku hiyo je! Wewe unayo hiyo shahuku? Kumbuka heri wenye kiu na shahuku maana hao watashibishwa .Daudi katika Zaburi ya 46 anasema kama “ayala waioneavyo shahuku maji ya mto divyo nafsi yangu ilivyo na haja nawe”.
Ndugu yangu na kuombea Mungu auishe hiyo shahuku ndani yako,Kama shahuku hiyo imepungua na muomba BWANA aiuwishe upya shahuku hiyo tena na tena.Mungu wetu ni Mungu wa mambo makubwa kwahiyo na wataka wakristo wote duniani kutokuwa legelege.
Shahuku yako kwa MUNGU isiridhike na mambo madogo madogo,chonde chonde shahuku yako kwa Mungu isiwe ni ya kuridhika na kutosheka haraka,kwa hiyo Zakayo anatufundisha kuwa na shahuku ya kudumu .
Kma shahuku hiyo kwako inasusua tafadhali nguvu ya msalaba iliyo mfufua Yesu krsto iambatane nawe sasa.
Jambo jingine amabalo Zakayo anatufunza siku ya leo ni hatua ya IMANI,Zakayo mara baada ya kumuona YESU aliamua kupanda juu ya mti na hatimae akamuona YESU.Ili imani yako ifanye kazi ni lazima uchukuwe hatua, na hatua za IMANI ni kudhubutu.
Mpendwa unapaswa kuwa shujaa wa IMANI kama Zakayo ambae alifanya mambo makubwa ambapo watu wasiojua walimcheka ila yeye moyoni alitambua kilichopo ndani yake na hatimae akafanikiwa.
Kazi ya imani yetu lazima itawaliwe na matendo, na matendo huja baada ya kudhubutu na hatimae hupata matunda.Tafadhali tena na tena nakusihii chukuwa hatua za IMANI.
2.KANUNI YA BATHIMAYO KIPOFU, moja kwa moja aliamini kuwa KRISTO anaweza pili anatufundisha yatupasa kumuita KRISTO bila kujali watu wanasemaje,tena bila kuchoka wala mashaka au wasiwasi wowote.Tumia wakati wako kumuita MUNGu.
3.KANUNI YA UAMSHO,fahamu uamsho unatangulia urejesho,na baada ya uamsho ndipo urejesho hiyo ndiyo tafsiri yake.Ili tusiyakose majira haya yatupasa kuyaweka maisaha yetu katika mstari.
MWISHO
Nakuatakia sikuku njema mpendwa na endelea kuitembelea www.mwakasegeinjili.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni