Jumatano, 23 Aprili 2014
MWANAMUZIKI NYOTA WA MAREKANI AELEZA ALIVYOSOTA LAKINI HAKUMUACHA MUNGU
James akiwa na kundi lake wakimsifu Mungu ndani ya Ruach city centre Kilburn jijini London jana.
Mwanamuziki nyota wa injili wa nchini Marekani James Fortune hapo jana aliwaeleza wakristo waliofika katika hitimisho la kongamano la pasaka lililoandaliwa na huduma ya Ruach Ministries la nchini Uingereza chini ya askofu John Francis na mkewe Penny Francis na kufanyika katika kanisa lao la Kilburn kwamba amewahi kuishi maisha ya shida sana lakini Mungu alimvusha.
James alizungumza hayo wakati akiimba wimbo uitwao 'Live through It' ambao umebeba album yake mpya kwamba amepitia majaribu mengi ikiwemo kuishi bila makazi yeye na familia yake (watoto, na mkewe) kwa miezi saba, wakihangaika pa kuishi lakini wakati yakiendelea hayo, watu walikuwa wakimfuata wakihitaji maombi kutoka kwake jambo ambalo lilimshangaza kwakuwa hata yeye kwawakati ule, alihitaji maombi kama wao. James akaendelea kusema kwamba lakini alichojifunza kwa kitendo hicho ni kwamba bado Mungu aliambatana naye na uwepo wake ndani ya James ulijifunua kwa watu wengine.
Mwimbaji huyo alihitimisha kwakuwaambia mamia ya watu waliofika katika hitimisho hilo lililoambatana na tamasha la muziki kwamba haijalishi ni matatizo gani ya maisha wanayapitia, waendelee kusimama na kumtumainia Mungu, atawavusha salama. Kongamano hilo lililopewa jina la 'Put it On the Next Generation' lilikuwa na wahubiri kutoka nchini Marekani kama Mchungaji Samuel Rodriguez, Dkt Carolyn Showell, Mtume Andre Jones pamoja na wenyeji askofu John Francis na mkewe pamoja na wachungaji wengine wa kanisa hilo lenye matawi matatu jijini London.
Kwa upande wa waimbaji kwaya ya Ruach, wageni James Fortune na Fiya, True Gospel Singers kutoka Denmark, Emanuel Chinese church pamoja na kundi la madansa liitwalo The Saints.
Ndani ya Ruach City Centre Kilburn.
James alikuwa akiimba na kufafanua jambo.
Upande wa wanamuziki wakionekana kwa mbali huku wakiwa wamezingirwa na wanamuziki wa Ruach ambao walikubali mziki uliokuwa ukipigwa na kundi la James.
Baadhi ya watu waliokaa ghorofani wakienda sambamba katika musifu Mungu.
Baadhi ya watu wakiwa wamepanga foleni kununua CD mpya ya James pamoja na kupata saini yake.
Kwa mara nyingine tena nikapata nafasi ya kukong'oli picha na James Fortune ambaye pia alikuwepo kanisani hapo mwaka jana.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni