Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Kanisa la Mtakatifu John lililopo Blackpool Uingereza, lilijengwa mwaka 1844, bado linavutia.
KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo nchini Uingereza, moja ya taifa ambalo limesifika kupeleka wamisionari sehemu mbalimbali duniani kuhubiri habari njema za Yesu Kristo na habari hizo kuwafikia vyema wapelekewaji ambao wengi wao wamebadilisha maisha yao na kuamua kumfuata Kristo. Mbegu ya Waingereza hao imefanya kazi njema ambayo imezaa matunda bora ambayo hata sasa ni ushahidi katika mataifa hayo kwakuwa injili ya Kristo imesimama mpaka leo.
KWA TAARIFA YAKO pamoja na taifa hilo kuwa nambari wani katika kusamabaza injili ya Kristo, lakini kwasasa mambo ni tofauti katika taifa hilo ambalo awali misingi yake ilijengwa katika Kristo nasasa ni mabadiliko makubwa kwani asilimia 70 ya wakazi wa nchi hiyo kwasasa hawaamini uwepo wa Mungu, zaidi ya kuamini mambo ya kisayansi jambo ambalo limesababisha hata mahudhurio makanisani ni hafifu hususani kanisa Anglikana ambalo ndio kanisa mama nchini humo ambalo naweza sema ni kanisa ambalo lina majengo mazuri sana yaliyotunzwa toka enzi hizo mpaka sasa yakiendelea kuwa na mvuto wa kipekee ndani na nje ya majengo hayo.
KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa taarifa kutoka katika moja ya vyanzo vya habari vya kanisa Anglikana la nchi hiyo ni kwamba takribani makanisa 20 hufungwa kila mwaka na majengo yake kugeuzwa kwa matumizi mengine kulingana na mnunuaji anavyoamua ama mkodishaji wa jengo, pamoja na wananchi wasehemu husika. KWA TAARIFA YAKO jambo hili limekuwa lakawaida sana kwa miaka ya karibuni katika nchi hiyo, ambapo makanisa ambayo hufikiriwa kufungwa hupelekwa wachungaji katika makanisa hayo ili kuvuta watu kuja kusali endapo lengo halitatimia la watu kuitikia mwito basi kanisa hilo hufungwa na jengo kuingizwa mnadani chini ya usimamizi wa kanisa kwa matumizi mengine lakini pia mtumiaji wa jengo hutakiwa kulitunza kwa ajili ya kumbukumbu ya vizazi vijavyo kama ilivyoada ya Waingereza.
Kanisa kuu Anglikana maarufu, la Durham Cathedral lenye miaka takribani 1000 toka lijengwe bado imara na linavutia wengi.©Wikipedia
KWA TAARIFA YAKO katika kufanya juhudi za kuwarejesha waumini kanisani, dayosisi za kanisa hilo hufanya maarifa wanayodhani yakazaa matunda, moja wapo ni kanisa la Mtakatifu Margaret lililopo King's Lynn waliamua kufungua mgahawa wa McDonalds kanisani hapo ili kuvutia vijana na waumini wengine kurudi kanisani, lakini pia kama haitoshi kuna makanisa ambayo hayapo mbali na baa ili kuwapa fursa waumini wake wanaopenda kutumia vileo kuingia katika baa hizo baada ama kabla ya ibada.
Kanisa likiwa na bango la Mgahawa wa McDonalds yote haya ili kuvutia waumini.
KWA TAARIFA YAKO wiki iliyopita nilihudhuria ibada ya kumuaga mchungaji msaidizi katika kanisa ninalosali maeneo ya Kensington magharibi mwa jiji la London, mchungaji huyu amekuwepo kanisani hapo kwa miaka mitano na ndiye alikuwa mshauri wangu wa kiroho hasa baada ya kufahamiana naye kwamba aliwahi kuishi Tanzania kwa miaka kadhaa, lakini pia kama haitoshi ni kati ya watumishi ambao wanamwamini Kristo, mchungaji huyu amehamishiwa huko Hastings kwakuwa kuna kanisa ambalo linahitaji mwamko kiupya hasa kutokana na kuwa na waumini 30 tu tena ni wazee ambao ibada zao zinaendeshwa kitamaduni zaidi. KWA TAARIFA YAKO lengo la mchungaji huyo kuhamishiwa huko ni kuokoa kutofungwa kwa kanisa hilo, endapo basi mwitikio utakuwa mzuri (kitu ambacho GK inakiombea kwamba Mungu akatende jambo) kanisa hilo halitafungwa.
Kanisa la Mtakatifu Bartholomew's katika mnada. soma orodha ya makanisa yanayouzwa kwasasa chini
KWA TAARIFA YAKO mdau wa GK unapopata taarifa kama hizi ni wakati wako wewe kulikumbuka taifa hili katika maombi maana baada ya miaka michache ijayo endapo mambo hayatabadilika basi utakuja kusikia asilimia 90 ya makanisa yote yamefungwa na majengo yanatumika kwakazi nyingine. Omba kwamba Mungu akafufue kazi yake kwa upya katika nchi hii ambayo kwasasa wachungaji na wahubiri kutoka Afrika ndio wenye makanisa makubwa ya kiroho ambayo waumini wake pia asilimia 90 ni kutoka Afrika ama visiwa vya karibeani.
Kanisa la Durham Cathedral ambalo GK liliwahi kupata nafasi ya kuabudu katika ibada ya usiku mtakatifu mwaka 2010 ©wikipedia.
Ifuatayo ni orodha ya makanisa yaliyowekwa kwenye tovuti ya kanisa Anglikana Uingereza tayari kuuzwa mwaka huu.
Kanisa la Durham Cathedral ambalo GK liliwahi kupata nafasi ya kuabudu katika ibada ya usiku mtakatifu mwaka 2010 ©wikipedia.
Ifuatayo ni orodha ya makanisa yaliyowekwa kwenye tovuti ya kanisa Anglikana Uingereza tayari kuuzwa mwaka huu.
Diocese | Location | Name | Contact |
---|---|---|---|
Manchester | Bacup, Lancashire | Bacup St John | Peter Townley |
Manchester | On Rishton Lane to the south of Bolton town centre (BL3 2BN) | Bolton le Moors St Simon and St Jude | Longden and Cook Commercial |
Manchester | Just off Bury New Road (A56) close to Great Clowes Street | Broughton St John | Longden & Cook Commercial |
Exeter | 1.5 miles north of outskirts of City of Exeter | Cowley St Anthony | Toby Perry |
Durham | Middleton St George, Darlington, DL2 1AP | St Laurence’s Church, Middleton St George | GSC GRAYS |
Manchester | On St James’ Street in Farnworth, Bolton (BL4 9SJ) | New Bury St James | Longden and Cook Commercial |
Manchester | Smallbridge, Rochdale, Lancashire | Smallbridge St John | Peter Townley |
Truro | Tregolls Road, Truro TR1 1ZQ | Truro St Paul | Mr Duncan Ley |
Chichester | Athelstan Road, Hastings TN35 5JE | Hastings All Souls | Oliver Dyer |
Worcester | St Georges Road, Redditch B98 8EE | Redditch St George the Martyr | A. Victor Powell (Chartered Surveyors) |
York | Acklam Road, Thornaby, Stockton-on-Tees, Cleveland TS17 7HB | Thornaby St Luke | GCS Grays (ref Calum Gillhespy) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni