Jumamosi, 19 Aprili 2014

NJOO UGUSWE UPYA TAMASHANI, YESU ALIKUFA KWA AJILI YAKO


Pastor Keke. ©Sunday World

Sasa yamebakia masaa machache kwa ajili ya kushudia namna Mungu anavyotukuzwa kwa njia ya uimbaji kwemnye tamasha la kimataifa la Pasaka, ambapo muimbaji mkuu ni Mchungaji Kekeletso Phoofolo (Keke) kutoka Afrika Kusini.


Jambo zuri ni kwamba Keke hatiokuwa peke yake, baadhi ya watumishi watakaokuwa pamoja naye siku hiyo ni Mama Mchungaji Sarah K kutoka nchini Kenya, (ataabudu pamoja nawe hadi useme ndio). Historia ya maisha yake yenyewe ni ushuhuda, kutoka uuzaji wa mboga mboga na hata kukatishwa tamaa na rafiki zake wa karibu, hadi kuinuliwa na Mungu kwa kuwa hakukata tamaa. Bofya hapa historia ya maisha yake.
Ama pia unaweza kusoma maswali ambayo ameulizwa na wasomaji wa Gospel Kitaa na Gospel Celebration, mengi usiyoyajua, pitia hapa.


Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, ni muimbaji ambaye kwa hakika sina shaka kukubali ajiitavyo, mtoto wa Tanzania (Son of Tanzania). Sekeleti amekuwa muimbaji wa nje ya Afrika Mashariki ambaye amekuwa sehemu ya jamii ya Watanzania, kutokana na kuwepo mara kwa mara kwenye matamasha mbalimbali. Historia ya uimbaji wake ni ushuhuda tupu, kwani hakuwa na ndoto ya kuwa muimbaji, ila ni mapatano na Mungu, kwani alimuomba kwamba, iwapo atamponya tatizo alilokuwa nalo kooni, basi atamtumikia Mungu kwa uimbaji. Soma hapa kujua zaidi.


Na upande mwingine tunakutana na Solomon Mukubwa, huyu ni muimbaji kutoka Congo ambaye anaishi Kenya ilihali roho yake ikiwa Tanzania. Kama hujaelewa maana yake, hebu bofya hapa kufahamu zaidi. Pamoja na hayo, Historia ya muimbaji huyu, ikiwemo namna ambavyo mkono wake ulikatika, ni wa kipekee. Habari hiyo inapatikana hapa kwa taarifa yako.

Solomon Mukubwa atakuwepo Mwanza, sanjari na Rebecca Malope, pamoja na Anastazia Mukabwa. Tuungane baadae kwa taarifa zaidi kuhusiana na tamasha hili la kimataifa la pasaka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni