Alhamisi, 24 Aprili 2014

EMMY KOSGEI AKANUSHA KUOMBA TALAKA NA MGAWANYO WA UTAJIRI WA MUMEWE


Mwimbaji nyota Emmy Kosgei wa nchini Kenya ambaye ameolewa na mtume Anselm Madubuko wa Nigeria, amekanusha vikali taarifa zilizotolewa na blog mbalimbali za nchini Kenya kwamba anadai talaka kutoka kwa mumewe ikiwa ndio kwanza miezi sita toka wafunge ndoa yao.
Emmy ambaye kwasasa yupo Boston nchini Marekani kwa ziara ya kihuduma, amesema bloggers wanaosambaza maneno hayo wamekosa kazi za kufanya. Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na gazeti Dailynation la Kenya zinasema bloggers hao katika taarifa zao wanadai kwamba mwimbaji huyo ameanza kudai talaka kutoka kwa mumewe sambamba na kutaka mgawanyo nusu wa utajiri wa mumewe huyo ambaye wanatofauti ya miaka 20 baina yao.

Emmy ni mmoja kati ya waimbaji nyota wa injili nchini Kenya ambaye toka ameanza kutoa album
zake za injili ambazo amekuwa akiimba sana lugha ya kwao pamoja na ubunifu wa mavazi yake na kundi lake zimekuwa zikipokelewa vyema na kumfanya apate mialiko mingi ndani na nje ya nchi yake ya Kenya.

Ambapo hivi majuzi ameachia video mpya katika album yake ijayo ikiwa kama utangulizi. Mdau wa GK kwa taarifa hii, si ya kusoma na kuiacha hewani cha muhimu ingia magotini umuinue mtumishi huyu wa Mungu aendelee kusimama katika ndoa yake na maneno yote yasemwayo juu yake basi shetani asijiinue na kuharibu huduma yake ambayo imefanyika baraka kwa wengi.

Emmy Kosgei siku ya harusi yake na mtume Madubuko wa Nigeria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni