Ashukuriwe MUNGU muumba mbingu nchi an dunia kwa
kutukutanisha tena siku hii ya leo katika blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com kwa ajili ya kusudi lake.
Jioni ya leo nakuletea mafundisho yaliyohubiriwa
siku ya leo katika kanisa la VICTORY CHRISTIAN CENTRE T.A.G lilopo hapa mkoani
Arusha eneo la Morombo.
Mwalimu ni Mch.Aloyce Mbughi.
Kanisani maana yake ni kusanyo la
watu waliokoka ambapo huweza kuwa popote pale hata kama ni chini ya mti.
Mimi na wewe ndio kanisa,wala si
jengo,mchungaji Mbughi anaelezea jinsi alivyoanza kanisa katika wakati mgumu kwani
alikuwa mwenyewe na wakati anaza huanza kwa ibada kama wako wengi kwani husema
“ tuanze ibada,tusimame” huku akiwa mwenyewe.
Siku moja watu walikuwa wakimjadili
ya kwamba “kuna kijana mmoja yuko pale kanisani (jengo la shule) na yuko kama
kichaa,na ukimkuta njiani ni mzima ila akiingia pale anakuwa kama kichaa.
Siku nyingine wakina mama
wakakubaliana waende kumsikiliza mtu huyu waliodai ya kuwa ni nusu
kichaa,wakati akihubiri bila kujua kumbe nje kuna watu waliokuwa
wakimsikiliza,siku hiyo alikuwa akihubiri juu ya Lazaro na yule tajiri.
Wakati wakuita watu na kuongoza sala
ya toba alikuwa akiongoza kwa kuacha
nafasi mithili ya mtu akiwa akimfatisha wakati akiomba na kukemea vifungo vya
shetani.
Mara akasikia kishindo cha mtu
akianguaka,kumbe miongoni mwao mmoja wao pepeo lilimtoka,alilazimika
kumkimbilia na kwenda kumuhudumia,hapo ndipo watu waliongozana nae na kuwahubria
INJILII.
Siku hiyo aliongoza sala ya toba kwa
watu watatu,ndipo alipoanza kufundisha somo ijpya la kukulia uokovu,kwa furaha watu walitangaziana ya kwamba “sio
KICHAA alafu ni MCHUNGAJI”,siku ya ijumaa kanisa lilisheheni watu kama 20.
Siku hiyo alishuhudia nguvu za Mungu
za ajabu,kwa muujiza baadae aliitwa kupewa kiwanja na serikali ya kijiji huko
Kibaha eneo la Tumbi alipewa heka 3 kwa shlingi 80,000 ts/= .
Leo kanisa lile lina kiwanja kikubwa mno na kumbuka lilianzia darasani na
mtu mmoja yani mchungaji tuu.
Sasa fahamu mambo makuu
3 yalipasalo kanisa kufanya;
1.Kumfanyia MUNGU ibada.”Ndio maana
jumappili,jumatano na ijumaa hukutana kwa ajili yakumwabudu yeye”,hata leo hapa
kanisani katika siku hii ya PASAKA tupo kwa ajili ya kufanya hivyo nawe wakati
huu unapo soma habari hii unaungana nasi katika kumuabudu yeye aliye mkuu.
2.Kumngoja BWANA,wakati tunamwabudu
Bwana tunapaswa kuufahamu kanisa ya kwamba Yesu nakuja kulichukuwa kanisa ,soma
zaidi 1petro 1:15,Yohana 14:1-6.Katika kungoja Bwana yatupasa kungoja katika
hali ya utakatifu tukijua pale alipo yeye yatupasa nasi kuwepo,hapa duniani
hata kama tusipo thaminiwa yatupasa kukumbuka ya kwamba pale aliopo ndipo
tutakapo kuwepo nasi,kumbuka ya tupasa kumngoja.
3.KUTIMIZA AGIZO KUU,tunao wajibu wa
kuabudu sawa,kumngoja katika hali ya utakatifu sawa,lakini pia yatupasa KUTIMIZA
AGIZO KUU,Maana yake ni kupeleka habari njema kwa watu ambao hawajampokea YESU
kama BWANA na mwokozi katika maisha yao.; mathayo
28:18-20 Yesu akaja kwao akisema kuwa nimepewa malaka yote duniania na
mbinguni basi enendeni mkayafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba la
Mwana na la Roho Mtakatifuna kuwaagiza kuyashika yote niliyo waamuru ninyi na
tazamamimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari.
Pia waweza kusoma katika kitabu cha
Marko 16:15-16.Wakati kanisa linatimiza agizo kuu linamfanya MUNGU atembe nao
kwa kiwango kikubwa “natazama mimi ni pamoja nayi siku zote hata ukamilifu wa
dahari” kwa hiyo kwa kufanya hivyo MUNGU atakuwa nasi hadi mwisho; kwa mantiki
hiyo tusipo fanya hivyo Mungu hawezi kutembea nasi kikamilifu.
Uinjilisti umegawanyika katika makundi makuu mawili ambapo la kwanza ni Uinjilisti
wa mtu kwa mtu au nyumba kwa nyumba mara zote huwa ni Huduma kwa wote,huweza
kufanyaka katika eneo lako la bishara,mashuleni au pale unapoishi kwenye basi
au kwenye shuhuli mbalimbali.
Kama umekuwa haufanyi hivyo tafadhali
fanya hivi sasa kwani Huduma hii ni ya umuhimu na usipofanya hivyo dhambi zao
zitatakwa kwako,usikubali kuwaona watu wakiangamia katika dhambi ungali na
uwezo wa kuwasaidia wao kuondokana na
dhambi zinazo wasonga.
Huduma hii haina Gharama wala haihitaji
muda mwingi au maalumu kwani huweza kuifanya popote,tofauti na itakayofwata
kwani hata wakati wakula chakula au kupiga
gumzo popote huweza kufanya hivyo.Katika hili hakuna “ubize” kwani hapo hapo
ulipo wanadamu unaoishinao hao hao
waweza kuwahubiria INJILI.
Unaweza ukatumia mabango,”stika”
ambazo zina ujumbe wa MUNGU ambao
kwanamna moja au nyingine huwa na nguvu ya uokovu.
Je! Ni watu wangapi hadi sasa ambao
wamesimama katika safari ya imani
kutokana na injili uliyowahubiria? Ongera kama wako,ila kama hawako
tafadhali anza leo nawe uliefanikiwa kufanya hivyo vyema endelea kufanya kazi
hiii NJEMA kwani ipo taji yako.
Kuhubiri kumbuka hakuna ufundi hakiki
hili kupitia kitabu cha 2wafalme 2:2-5 Ona
binti huyu alivyo sema “laiti kamaa bwana wangu angalikwepo kule kwetu
angalipona” Watu waliosikia hizi habari walitambua ya kwamba uwezekano wa
kupona kwa shujaa wao upo.
Je! Wewe unashindwa kuwambia watu ya
kwamba YESU akiingia ndani yako ulevi utakwisha au yakushinda kumweleza mlevi
ya kwamba laiti kama ungalikwepo kwetu tuliokoka angali acha ulevi” hayo tuu
yatosha kuubadilisha maisha ya mwenye dhambi.
Kile unachokijua kuhusu YESU kiseme
YOHONA 4:28 Basi Yule mwanamke akauacha mtungi wake akaende mjini akawaambia
watu njooni mumuone mtu aliyeniambia mambo yote niliyowahi kuyatenda Je1
hamkini huyu ndiye KRISTO.
Hii haikuhiitaji kozi wala ufundi.
Tazama tena LUKA 8:38-93 Na mtu Yule aliyetokwa na pepo alimuomba ruhusa
afwatanane nae lakini yeye akamwambia “rudi ukawaambie watu matendo makuu MUNGU
aliyokutendea” Mtu huyu alikuwa Ushuhuda
mkubwa kwa watu wengi.
Kumbuka sehemu ya pili katika agizo
kuu ni Huduma ambao mara nyingi hufanyika katika makutano makubwa ya watu au
vyombo vya habari.
Kwa habari kama hii
tafadhali endelea kutemelea hapa www.mwakasegeinjili.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni