Jumatatu, 7 Aprili 2014

NYOTA WA MUZIKI WA INJILI NCHINI KENYA AFARIKI DUNIA


Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Kenya aliyetamba na wimbo wa 'Kiburi ni chanini' aitwaye Peter Kahura Kaberere amefariki dunia baada ya kupigwa shoti ya umeme akiwa kwenye eneo lake la kusafisha magari siku ya jumapili.

Mwimbaji huyo ambaye pia alikuwa meneja wa kampuni ya Mo Sound Limited ambayo pia inasimamia tuzo maarufu za nchini humo za Groove, alipatwa na umauti wakati akisafisha gari lake tayari kuelekea kanisani eneo la Lower Kabete lakini kukawa na hitailafu ya umeme kwenye mashine ya kuoshea gari ambayo ilisababisha umeme huo kumkausha na kukutwa sakafuni na mkewe akiwa amekufa.

Taarifa za kifo cha mwimbaji huyo zilitolewa na mkewe kupitia ukurasa wa Facebook wa mwimbaji huyo na kufuatiwa na salamu mbalimbali za rambirambi kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wapenzi wa muziki wa injili. Taarifa hizo ziliendelea zaidi kupitia ukurasa wa Facebook wa tuzo za Groove ambao pia ujumbe wao uliandikwa kuonyesha ni kwa jinsi gani wamehuzunishwa na kifo cha mwimbaji huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni