Jumamosi, 12 Aprili 2014

ALEX MSAMA APATA AJALI YA GARI, ALAZWA MUHIMBILI


Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, katika tamasha la kimataifa la Krismasi mwaka 2013.

Mkurungenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Bwana Alex Msama amepata ajali ya gari siku ya jana majira ya saa tano asubuhi mkoani Dodoma.
Hali yake inasemekana inaendelea vizuri..
Taarifa Mpya, Jumamosi mchana
Tayari kwa mujibu wa familia, Bwana Msama, ambaye kupitia kampuni ya Msama Promotions, ndio huandaa matamasha ya kimataifa ya injili kwa muziki, amehamishiwa hospitali ya taifa ya Muhimbili, ambapo imeelezwa kuwa ana michubuko maeneo ya kifuani na mkononi.

Hivi sasa maombi yako yanahitajika.
Taarifa zaidi zitaendelea kukujia kwa kadri ambavyo GK itakuwa ikizipata, endelea kufuatilia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni