Jumatano, 23 Aprili 2014

MTEKAJI NYARA AAMUA KUMUACHIA MTOTO ALIYEMTEKA BAADA YA MTOTO KUMWIMBIA MUNGU BILA KUCHOKA


Willie akifanyiwa mahojiano katika moja ya radio huko Atlanta kwa ushuhuda wake.
Mtoto mvulana wa miaka 10 amepata muujiza wa ajabu baada ya kunusurika kuchukuliwa na watekaji ambao walishampakiza ndani ya gari lakini kitendo chake cha kuimba wimbo uitwao 'Every Praise' kwa Mungu utunzi wake Hezekiah Walker muda wote akiwemo ndani ya gari licha ya kukatazwa kufanya hivyo, kilimfanya dereva wa gari hilo kuamua kumuachia kutokana na kelele za uimbaji za mtoto huyo ambazo Mungu alizisikia na kumponya kutoka mikononi mwa majangili hayo.

Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Willie Myrick alihadaiwa kupewa pesa iliaingie ndani ya gari


Mchoro wa mtekaji iliyotolewa na askari wa Atlanta.
hilo la mtekaji alipokutwa nje ya nyumba yao huko Atlanta Georgia, lakini kijana huyo hakuwa mrahisi kuingia garini ndipo mtekaji huyo alipoamua kumkamata na kumpakiza garini, lakini katika mwendo wa masaa matatu ndani ya gari hilo akimwimbia Mungu wimbo huo wa 'Every Praise' wenye maneno kama 'God my Saviour, God my Healer, God my Deliverer, Yes He is' kilimkera mtekaji na kuamua kumfungulia mlango na kumuachia huku akimwambia asimwambie mtu yeyote kuhusu jambo hilo.

Willie alitoa ushuhuda wake kanisani uliomfanya mwimbaji na mtunzi wa nyimbo maarufu nchini Marekani Hezekiah Walker alisema anataka kumkumbatia mtoto huyo kwa ufunuo wake wa kumtukuza Mungu katika jaribu alilokuwa nalo. Tayari askari wa jimbo hilo wameachia mchoro wa mtu anayedaiwa kuhusika na tukio hilo ambalo kijana Willie alizungumza na runinga ya WXIA-TV. Habari hii imetangazwa na kuandikwa kwenye vyombo mbalimbali likiwamo gazeti la METRO la jijini London nchini Uingereza linalotoka kila siku asubuhi jumatatu hadi jumamosi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni