Jumatano, 30 Aprili 2014

HABARI PICHA KUTOKA MBEYA: MAZISHI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA WANAWAKE WA INJILI EAGT


Picha ya marehemu Mama Benja (Junitha B. Mwamnyila)

Shujaa umekwenda, Kazi umemaliza mama kapumzike, ni baadhi ya maneno yaliyosikika na GK kwa waombolezaji waliojitokeza katika viwanja vya kanisa la EAGT Gilgal Mwanjelwa kuuaga mwili wa Mwinjilisti na Mkurugenzi wa WWI Taifa Mama Benja na kisha kwenda kuulaza kwenye nyumba ya milele maeneo ya Sabasaba.


Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri kama ambavyo GK iliahidi kukuletea baada ya kupiga kambi msibani hapo, ambapo awali ilikupa picha za awali.

VIONGOZI WAKUU WA EAGT TAIFA NA WACHUNGAJI



















Mchungaji Daniel Kulola



MKE WA MAREHEMU MOSES KULOLA NAE ALIKUWEPO







WATOTO NA NDUGU WA MAREHEMU MAMA BENJA













MARAFIKI WALIKUWEPO KUFARIJI







WATU MBALIMBALI WALIJITOKEZA KUAGA
















WENGINE WALISHINDWA KUJIZUIA




















MWILI ULISHUSHWA KABURINI












MAVUMBINI TUTARUDI






Marehemu ameacha watoto wanne, ambapo uzao wake wote umekuwa watoto mapacha, mara ya kwanza akijifungua mapacha wa kike, na kisha uzao wake wa pili ukiwa mapacha tena, wa kike na wa kiume. Na katika maisha yake, Mama Benja (Benjamin likiwa jina la marehemu mume wake aliyekwisha fariki miaka mingi iliyopita) amekuwa mwinjilisti hodari na kushika nyadhifa mbalimbali kwenye kanisa la Evangelistic Assemblies of God.


Kama hukupata fursa ya kusikia maneno yake ya mwisho, basi bofya hapa, usikie alichosema marehemu ambaye alizaliwa tarehe 2 Oktoba 1951, na kufariki dunia tarehe 24 Aprili 2014. Kwa watumiaji wa simu bofya hapa kuipakua. Gospel Kitaa inawaombea wafiwa wote wapate nguvu katika kipindi hiki kigumu. BWANA ametoa, na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.

Jumapili, 27 Aprili 2014

CHRIST WORSHIP HOUSE CELEBRATION CONFERENCE

Christ Worship House inaanza kivingine mwaka huu - kwao mwaka 2014 ndio mwaka wa celebration. Upo maeneo hayo? Basi usichelee, jiunge nao ambapo tarehe 28 April hadi 2 Mei watakuwa na kongamano, ambalo litafuatiwa na Live Recording tarehe 3 na 4 Mei.