Jumatatu, 30 Septemba 2013

ONAJINSI WALIOCHUKULIWA MSUKULE WALIVYO RUDI KWA MAOMBI ARUSHAM NA Mchungaji Gwajima

MWANAMKE ALIYEKUFA MIAKA MINGI ARUDI MKUTANONI ARUSHA WATOTO WAKE WAZIMIA BAADA YA KUMTAMBUA

Mama wa kwanza kushoto anayedaiwa kufariki siku nyingi akiwa mkutanoni na mwanamke mwingine ambaye pia alichukuliwa msukule, hapa ni baada ya kuanguka karibu na eneo la mkutano, kumbe watoto wake walikuwa mkutanoni pia.www.mwakasegebibilia.blogspot.com

SOMO LA Mwl. Christopher Mwakasege: Zijue Karama Za Roho Mtakatifu – II.


Mwl. Christopher Mwakasege

SEHEMU YA NNE Karama ya neno la Maarifa
I Wakorintho 12:4,8; ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima, na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule”.

Kama tulivyo jifunza huko nyuma kazi ya karama ni kulijenga kanisa.
Kazi ya karama ya neno la maarifa.www.mwakasegebibilia.blogspot.com

SOMO LA Mwl. Christopher Mwakasege: Zijue Karama Za Roho Mtakatifu – I.


Mwl. Christopher Mwakasege

I Wakorintho 14:12. Inasema ‘vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za rohoni, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. Mungu hafanyi kitu bila kusudi, na kusudi la semina hii ni:-
Kuna jambo Mungu anataka kufundisha katikati yetu ambalo litahusisha sana utendaji wa karama za Roho Mtakatifu.

Kurahisisha ujenzi wa kanisa lake na kazi zake. Mfano, kuna urahisi wa kujenga kwa kutumia mashine za kujengea na kubeba matofali kuliko kutumia mkono, ni sawa na kufanya kazi ya Mungu kwa kutumia karama za Roho Mtakatifu.www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Safu ya James Kalekwa: Umejenga Juu ya Mwamba au Mchanga? - Part II


James Kalekwa
Somo linaendelea....
Mwamba 1: Tawala nafsi yako kwa kuongoza milango yako ya fahamu.
Mithali 4:23
"Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima."
Ili uweze kusaidika juu ya habari ya nafsi ni muhimu sana kutambua na kukumbuka siku zote mwanadamu ni nani, wewe ni nani au ni kiumbe wa namna gani. Wewe niroho yenye nafsi inayoishi ndani ya mwili. Rejea kitabu cha Mwanzo 2:7, " BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai." Ambapo utaona mwanadamu ni muunganiko wa mavumbi ya ardhi, pumzi ya uhai na nafsi hai… Kwa msingi huo basi mavumbi ndiyo mwili, pumzi ya uhai ni roho na nafsi hai ni nafsi!www.hakileo.blogspot.com

Safu ya James Kalekwa: Umejenga Juu ya Mwamba au Mchanga?



James Kalekwa
Utangulizi wa somo:
Mathayo 7:24-27
“Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, afuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.”www.mwakasegebibilia.blogspot.com

ASKOFU SOLLO AMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA KUENDESHA NCHI KWA AMANI




HUKU nchini kenya hofu ya vitendo vya ugaidi vilivyofanywa na watu wanaosadikika kuwa kundi la wanamgambo wa al-Shabaab katika eneo la maduka ya bidhaa la Westgate mjini Nairobi ikiendelea kutawala nchini Kenya, askofu wa kanisa la maombezi na uponyaji cha Overcomers (OPC) mkoani Iringa Dr Boaz Sollo amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuendelea kuliongoza Taifa katika hali ya amani na utulivu na kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini kote nchini kujikita katika maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania amani ili yaliyotokea Kenya yasiikumbe Tanzaniawww.mwakasegebibilia.blogspot.com

HABARI PICHA, ARUSHA YAKOMBOLEWA, MAELFU WAMPOKEA YESU ktk MKUTANO BWA INJILI.

Kati ya siku ambayo wakazi wa Arusha walipata kufunguliwa dhidi ya vifungo vilivyokuwa vinawasumbua, basi ni siku ya Jumapili ambapo mkutano mkubwa ulioandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima umefikia siku ya tatu.

Wakazi hao walioanza kufurika kwenye viwanja vya reli kutoka kona mbalimbali ya mji huo, hatimaye walipata chakula cha kiroho na kufunguliwa kwa mamlaka ya Jina la Yesu. Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio la mkutano huo ambao Gospel Kitaa ilipata fursa ya kuwepo na kushuhudia namna ambavyo Mungu anatumia watu wake kuponya wenye shida na matatizo

Siku ya 4 ya mkutano Mchungaji Gwajima atahubiri kuhusu aina za misukule. Usikose kuhudhuria kwani mwisho wa mkutano huu wa wiki mbili, utapata uwezo wa kutambua aliyefariki na aliyechukuliwa kwa njia za ajabu.
.
Mchungaji Gwajima akihubiria maelfu ya wakazi wa Arusha na waliojitokeza kumpoke Yesu kuwa mwokozi wa maisha yao.
 
Mara baada ya kuongozwa sala ya toba, wakarejea kwenye viti vya, ambapo walitakiwa kuendelea kupata huduma kwenye kanisa lolote la kiroho linalomhubiri yesu na kunena kwa lugha.



jacson Benty akimuabudu Mungu kabla ya maombi kuanza.www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Jumamosi, 28 Septemba 2013

VIONGOZI WA KIDINI KENYA KUONGOZA MAOMBI YA KITAIFA JUMANNE


Rais Uhuru Kenyatta na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la mpwa wao marehemu Mbugua Mwangi na mchumba wake Rosemary Wahito ambao waliuawa katika tukio hilo la kigaidi. Picha na Daily Nation Kenya.
Viongozi wa kidini nchini Kenya wanatarajia kufanya maombi kwa taifa lao siku ya jumanne ijayo katika viwanja vya KICC kuanzia majira ya saa nne asubuhi. Akitoa tangazo hilo katibu mkuu wa taasisi ya jumuiya ya Kikristo nchini humo National Christian Council of Kenya (NCCK) bwana Peter Laranja amewataka watu kutoka madhehebu yote pamoja na viongozi wa dini zote kukutana hapo kwa ajili ya kuiombea Kenya.

BABU WA LOLIONDO AIBUKA TENA


Ambilikile Mwaisapila ‘Babu wa Loliondo’.
Na Mwandishi Wetu:



MCHUNGAJI mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapila ‘Babu wa Loliondo’ amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na baadaye kioo cha dunia. Ametoa kauli hiyo Septemba 24

MASANJA MKANDAMIZAJI HIVI SASA YUKO MAREKANI KUHUBIRI


Masanja alipokuwa jijini New York alipokwenda kwa mara ya kwanza.
Mungu ameendelea kufungua milango kwa mchekeshaji wa kundi la Original Comedy ambaye pia anafanya kazi za kumuhubiri Mungu kijana Emmanuel Mgaya au mwite kwa jina lake la kazi Masanja Mkandamizaji ambaye kwasasa yupo nchini Marekani kwa huduma ya kimungu ambako amealikwa kwa kazi hiyo ikiwa pamoja na kuzungumza na vijana katika miji mitatu ya California, Minnesota pamoja na Dallas.
Je, unafahamu uzuri wa Mbinguni?

Mpendwa msomaji, kwanza pole sana na shughuli nyingi za kila siku. Ninajua kwamba muda wako ni mchache sana, kutokana na shughuli zako nyingi. Hata hivyo ninakuomba muda wako mfupi tu, ili tuzungumze juu ya jambo muhimu ambalo nimeona kwanba ni vema nikushirikishe. Je umekubali ombi langu? Natumaini umelikubali. Asante sana. Basi ninakusihi tufuatane pamoja katika mazungumzo haya.


Huenda utakuwa umewasikia watu wengi waliofiwa na ndugu, jamaa au marafiki zao wapendwa, wakisema, ”Mungu waweke mahali pema peponi“. Jambo hili linadhihirisha jinsi kila mmoja wetu anavyoamini kwamba kuna mahali pema peponi yaani mbinguni. Na tena inaonyesha jinsi sisi sote na jamaa zetu tunavyopenda kwenda huko. Je,wewe una shauku ya kwenda mahali pema peponi au mbinguni, baada ya kuiaga dunia hii? Najua wewe pia una shauku ya kwenda mbinguni siku moja. Hata hivyo, shauku yako itaongezeka zaidi utakapokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu uzuri wa mbinguni. Peponi au mbinguni, ni wapi na kukoje? Peponi au mbinguni, kuna uzuri usioweza kufananishwa. Tukifahamu jinsi mbinguni kulivyo kuzuri, kila mmoja wetu atazidi kuwa na shauku ya kufika huko siku moja. Tufuatane basi ili upate ufahamu wa kutosha kuhusu mbinguni au peponi.

HISTORIA YA UIMBAJI NA MUZIKI



Na Mwl Christopher Frank

Uimbaji asili yake ni mbinguni (Eze 28:13-15). Tutakapofika mbinguni tutaendelea kumwimbia Bwana (Ufu 15:2-4; Ufu 5:9-10).

Hapa duniani nyimbo na muziki vilianza zamani sana baada ya kuumbwa kwa Adamu na Hawa "...na jina la nduguye  aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi."(Mwa 4:1-21).


UMUHIMU WA KWAYA KATIKA KANISA
Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja(na kupiga vyombo vya muziki). Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma ya uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za kuvutia na uwezo wa kutunga nyimbo  mpya. Kanisa ni mwili wa Kristo wenye viungo vingi; na kila kiungo kina kazi. Kiungo hiki (Kwaya) kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa litahudumiwa (1 Pet 4:10-11).

Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la Kale walikuwepo watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya 6:31-32). Maneno ya nyimbo yana nguvu kubwa. Yanaweza kubadili hali ya huzuni kuwa ya furaha na moyo mgumu kuwa laini. Mtu mwenye udhaifu anaweza kusikia nguvu na uzima kwa nyimbo. Daudi alipopiga muziki roho mbaya ilimwacha Sauli (1 Sam 16:23).  Tunasoma pia kwamba siku moja Sauli aliingiwa na ghadhabu, chuki na kumwonea Daudi wivu baada ya kusikiliza maneno ya nyimbo (1 Sam 18:6-9).



Ijumaa, 27 Septemba 2013

HARUSI KTK BWANA NI SIMON NA ASIGELE SONELO .



Shangwe za GK hii leo tunakwenda kwa mmoja wa waimbaji katika moja ya kwaya zinazofanya vyema sana katika tasnia ya uimbaji jijini Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla bwana Simon na mkewe Asigele Sonelo ambaye ni mwanakwaya wa Efatha ya Uhuru Moravian Kariakoo au waite wana wa "Twaomba Amani" au wana wa "Usalama", wapenzi hawa wawili walifunga ndoa yao iliyofana sana katika kanisa la Moravian Uhuru Kariakoo jijini Dar es salaam na kufuatiwa na sherehe kubwa ya kuwapongeza iliyonogeshwa na waimbaji wenzake wa Efatha pamoja na mwanamama Bahati Bukuku. Angalia baadhi ya picha mambo yalivyokuwa.


Matron mrs Nsajigwa au mwite Tupilike mama Victorio akipambwa.www.mwakasegebibilia.blogspot.com
Vazi rasmi la bwana harusi likisubiria kuvaliwa. 

Bwana Nsajigwa Richard akimweka sawa bwana harusi.

pigo,,MPIGA BASS NYOTA WA JOYOUS CELEBRATION ANUSURIKA KIFO


www.mwakasegebibilia.blogspot.com
Sabelo katika picha baada ya ajali.
Ikiwa siku ya jana na leo kundi la Joyous Celebration linafanya onyesho lake la nyimbo za zamani kwa kualika waimbaji waliowahi kuimba na kundi hilo, mmoja kati ya wapigaji mahiri waliowahi kutumika katika kundi hilo wakiwajibika katika gitaa la bass mwanakaka Sabelo Masondo amenusurika katika ajali mbaya ya gari alilokuwa akiliendesha.

Masondo ambaye ameachana na kundi la Joyous zaidi ya miaka mitatu sasa amepata ajali hiyo mbaya kwa gari alilokuwa akiliendesha aina ya pick up kupinduka zaidi ya mara sita nayeye akitoka na majeraha madogo ikiwemo kuumia sehemu ya jicho huku gari likiwa katika hali mbaya, katika ujumbe wake alioutoa katika ukurasa wake wa Facebook nyota huyo wa kuliungurumisha gitaa zito amemponda shetani kwakuimba wimbo maarufu uitwao "How great is our God" na kumwambia shetani kwamba Mungu ni mkuu na kwamba hatoweza kamwe kumsogelea ama kujilinganisha naye, na kwamba yeye Sabelo anasonga mbele daima.

Jumatano, 25 Septemba 2013

NINAMWAMINIJE TENA MTU ALIYENITOSA WAKATI WA TAABU YANGU?

hakileo.blogspot.com

Pastor Carlos Kirimbai
MIT. 25:19 SUV

Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.

Ngumu sana.

Yesu alisema haya maneno kwa wanafunzi wake waliyodumu pamoja naye hata katika magumu Yake.

LK. 22:28-30 SUV

Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

Wale watu wanaodumu pamoja nawe kwenye saa yako ya jaribu ndo wanaostahili kuingia nawe kwenye saa yako ya utukufu.

Magumu na majaribu yanakuja ili kukusaidia kujua umezungukwa na watu wa namna gani.

Wale wanaopita jaribio hilo ndo hasa wenye moyo wa kuwa na wewe katika safari yako ya kuelekea kwenye hatima ya Kimungu ilyoandaliwa kwa ajili yako.

Jumapili, 22 Septemba 2013

BWANA ANA HAJA NAWE. *sehemu ya nane*

Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana lipewe sifa…

Haleluya…
Nasema Haleluya…

Nimepewa kazi moja tu na Bwana Mungu,nayo ni kuhubiri injili kwa watu wote,sina kazi nyingine yenye maana ambayo inampa Bwana utukufu,
isipokuwa ni kuhubiri injili tu.
Ndio maana leo Bwana kalileta neno lake hili mahali hapa kwa sababu Bwana ana haja nawe,ndio maana upo hai mpaka hivi sasa.

Nawe umepewa fursa hii ya pekee ya kupitia ujumbe huu,ujue lipo kusudi la Bwana ya kwamba Bwana ana haja nawe.
Msingi mkuu wa fundisho hili umetoka katika kitabu cha Luka 19 :31
Karibu tuzidi kuendelea zaidi kufundishwa na Roho wa Bwana mahali hapa;

Luka 19:31

WAVUNJA KANISA KATOLIKI NA KUACHIA HAJA KUBWA MADHABAHUNI MKOANI PWANI



Watu wasiofahamika wameiba vitu kadhaa Kanisa Katoliki kigango cha Jaribu mkoani Pwani. 

Katekista wa kanisa hilo katoliki Joseph Mwiru kutoka Pwani anaeleza kuwa sanamu ya Bikira Maria, Msalaba, meza ya kusalia, na meza ya kuandalia vifaa, na kisha baada ya hapo kujisaidia haja kubwa sehemu tatu tofauti madhabahuni.www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Jumamosi, 21 Septemba 2013

SHETANI ANAONGOZA CHUKI DHIDI YA ISRAEL


"Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali YATAFAKARI MANENO YAKE MCHANA NA USIKU, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapofanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana." (Yoshua 1:8) Mtu mmoja aliwahi kuniuliza swali hili: "Je kutafakari maana yake nini?" Kila mara ninapofundisha somo hili nakutana na swali la jinsi hii . Naamini kuwa swali hili linawatatanisha wengi kwa sababu bado hawajatofautisha kati ya kusoma neno na kutafakari neno. Kusoma neno ni tofauti na kutafakari neno. Kulitafakari neno ni zaidi ya kulisoma neno. Watu wengi huwa wanasoma neno zaidi kuliko kulitafakari. Kutafakari maana yake nini? Maana ya karibu sana ya neno kutafakari ni kuwaza. Ni kusoma neno huku unalicheua na kulitafuna rohoni mwako. Kutafakari ni njia mojawapo kubwa ya kuweza kuilisha roho yako. Yesu Kristo alisema "Imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu." (Mathayo 4:4) Mkate ni chakula cha mwili wa nje ulio wa nyama na damu; neno la Mungu ni chakula cha mwili wa kiroho. Kinywa kinapokea chakula na meno yanatafuna.na kukivunjavunja huku kikilainishwa na mate, tayari kwa kumeza. Kusoma neno ni kama kinywa, kazi yake ni kulipokea neno. Kutafakari ni kuvunjavunja hilo neno huku Roho wa Mungu akililainisha liwe tayari kumezwa na roho yako. Kutafakari neno kunamletea mtu siri ya ajabu ya uhakika na ushindi ndani ya Kristo. 

SOMA HII,,Hafla ya Kuchangia maandalizi ya Usiku wa Kusifu na Kuabudu yafanyika Peacok Hotel




Paul Mwangosi wa pili akiimba sambamba na marehemu Fanuel Sedekia

Tanzania Praise and Worship Team ni kundi la kusifu na kuabudu linaloongozwa na Mtumishi wa Mungu Paul Mwangosi.Dhumuni kubwa la uwepo wa Kundi hili ni kumwabudu MUNGU katika ROHO na KWELI.Mnamo mwaka 2008 mmbeba maono wa Kundi hili mtumishi Mwangosi ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akihudumu kama kiongozi wa kusifu na kuabudu katika semina za Mwl Christopher Mwakasege alipata maono ya kuanzisha Kundi litakalokuwa likimsifu Mungu kwa namna ya kipekee.

Historia ya Mwanamuziki Donnie Mcclurckin


Pastor Donnie Mcclurkin

Donnie Mc Clurkin ni Mwanamuziki Mashuhuri wa nyimbo za Injili na Mchungaji wa Kanisa la Perfecting Faith church lililo katika jimbo la Detroit nchini Marekani.


Donnie alizaliwa na Familia ya Bw Donald Sr na Mama Frances Mcclurkin mnamo Jan 25 mwaka 1959 na kukulia katika mji wa Louisville. Akiwa na umri wa miaka nane(8), mdogo wake wa kiume mwenye miaka miwili(2) aligongwa na gari na kufa papo hapo huku Donnie akishuhudia.Wakati Donne akiwa na majonzi mazito usiku huo huo ambao walimzika mdogo wake, mjomba wake alimbaka Donne.



Baada ya kifo hicho familia yake iliingia kwenye mgogoro kubwa ambao ulitokana na utumiaji wa dawa za kulevya. Baada ya kufikisha miaka 13, binamu yake mtoto wa mjomba wake alimbaka Donnie pamoja na dada zake wawili kitendo amabacho kilimuumiza sana na kumuachiia kovu la aina yake. Muda wote alijiona mkosaji, mtu aliyekandamizwa na hakuwa na ujasiri mbele za watu na mwenye wingi wa aibu.

Ijumaa, 20 Septemba 2013

KESHO ILIYOCHELEWESHWA


Mchungaji Josephat Gwajima.
Utangulizi:

Hii ni sehemu ya pili ya somo la hatua iliyocheleweshwa. Ni muhimu kujua kuwa Mungu ni Mungu wa makusudi na hakuna kitu anachofanya pasipo kusudi. Mbele za Mungu; Maisha ya mtu hayaanzi tumboni mwa mama yake bali yanaanza kabla ya mtu kuwa tumboni yaani Mungu huyaona maisha ya mtu kabla ya kuwa tumboni. Kimsingi, Mungu anajua kesho ya mtu kabla haijafika; katika ulimwengu wa roho kusudi la maisha ya mtu laweza kuonekana.

MTOTO AFUFUKA BAADA YA MAOMBEZI


Mama Mzazi wa Dickson, Happiness Joseph alijikuta akibubujikwa na machozi ya furaha alipompokea mtoto wake akiwa hai baada ya maombi ya kumfufua kutoka kwa Mch. Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi la Kigoma, Paul Joshua.

Alhamisi, 19 Septemba 2013

What GOD plans to us and us to HIM.

Huu ndo mtazamo wa wengi wetu kwenye maisha ya kila siku, ingawa hatujui mambo gani yameepushwa. Ujumbe huu umenukuliwa kwenye mzunguko wa barua pepe.

Our perspective makes a difference. Enjoy the read.
How was your day?

Me: God, can I ask you a question?

God: Sure.
Me: Promise you won't get mad?

God: I promise.
Me: Why did you let so much stuff happen to me today?

God: What do you mean?
Me: Well, I woke up late.

God: Yes.
Me: My car took forever to start.

God: Okay.
Me: At lunch they made my sandwich wrong and I had to wait.

God: Hmmm.
Me: On the way home my phone went dead just as I picked up a call.

God: Okay.
Me: And on top of all that, when I got home I just wanted to soak my feet in my new foot massager and relax, but it wouldn't work!!! Nothing went right today! Why did you do that?

God: Well, let me see. The Death Angel was at your bed this morning  and I had to send one of the other angels to battle him for your life. I let you sleep through that.
Me: (humbled): OH...

God: I didn't let your car start because there was a drunk driver on your route that would have hit you if you were on the road.
Me: (ashamed) Oh ...

God: The person who made your first sandwich today was sick and I didn't want you to catch what he has. I knew you couldn't afford to miss work.
Me: (embarrassed): Ok...

God: Your phone went dead because the person who was calling was going to give false witness about what you said during that call. I didn't even let you talk to them so that you would be covered.
Me: (softly) I see, God.

God: Oh, and that foot massager had a short that was going to throw out all of the power in your house tonight. I didn't think you wanted to be in the dark.
Me: I'm sorry God.

God: Don't be sorry, just learn to trust me in all things, the good and the bad.
Me: I will trust you.

God: And don't doubt that MY plan for your day is always better than your plan.
Me: I won't, God. And let me just tell you God, thank you for  everything today.

God: You're welcome, child. It was just another day being your God, and I love looking after my children.

Share this and keep it going, someone out there needs it.www.mwakasegebibilia.blogspot.com

MKUTANO: MBULU KWA YESU, MKUTANO WA INJILI WABADILI JAMII

Hakuna jambo jema kwa muhubiri yeyote anapohubiri na kwisha mwisho wa siku watu wanaamua kukata shauri na kumpokea Yesu kama kiongozi wa maisha yao. Na hivi ndivyo Gospel Kitaa imeshuhudia wakazi wa Mbulu wakipata Neema ya kuhudumiwa kupitia mkutano ulioandaliwa na kanisa la PAG, ambao utaendelea hadi siku ya Jumapili.

Jumatano ilikuwa siku ya kwanza, na zifuatazo ni picha za kilichojiri siku hiyo.




Wakazi wa Mbulu wakifuatilia kwa makini na kupokea unabii kutokea jukwaani.

Charles Festo wa Manyara Band akiwajibika kumtukuza Mungu

Jumatatu, 16 Septemba 2013

HISTORIA YA ASKOFU MOSES KULOLA.


www.hakileo.blogspot.com

Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1930, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Ni mume wa Elizabeth na wamezaa watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.

Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.

Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.

ANGALIA INJILI NDANI YA JIJI LA KAMPALA UGANDA

www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Angalia kutoka mitaa ya jiji la Kampala nchini Uganda ambako GK ilipita na kufanikiwa kuingia katika moja ya makanisa maarufu nchini humo liitwalo Watoto ambalo makao makuu yake yanapatikana jijini hapo katika barabara ya Kampala huku kanisa hilo likifungua matawi zaidi mikoa ya nchi hiyo. Kanisa hili ndio nyumbani kwa kwaya maarufu duniani ya Watoto Children Choir, utaratibu wao wa ibada na uimbaji wao unalingana na ule wa kanisa la Hillsong ambalo pia hutoa misaada kwa kanisa hilo lililoanzishwa na Gary Skinner ambaye wazazi wake walikuwa wamisionary huko nchini Zimbabwe.

Pamoja na picha kutoka katika ibada hiyo katika kanisa la Watoto GK pia ilipita mitaani na kuona wainjilisti wengi wakujitolea wakipiga gombo lakini kamera ikafanikiwa kuwanasa wawili tu mmoja akiwa mitaa ya jinja road na mwanadada yeye alikuwa maeneo ya Entebbe akipiga injili, wote kwa pamoja walikuwa wakitumia lugha yao ya kiganda.


Ijumaa, 13 Septemba 2013

PADRI Anselmo AMWAGIWA 'TINDIKALI' ZANZIBAR




Padri Anselmo Mwang'amba baada ya tukio la kumwagiwa tindikali.

Taarifa ambazo Gospel Kitaa imezipata kwa ufafanuzi ni kuwa Padri wa kanisa katoliki visiwani Zanzibar amemwagiwa maji yanayodhaniwa kuwa ni tindikali.

Kwa mujibu wa WAPO Radio FM kupitia kipindi chake cha Yaliyotokea jioni hii, Padri Anselmo Joseph Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, mkoa wa mjini magharibi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, alikuwa internet café majira ya saa tisa alasiri maeneno ya Mlandege.

Jumanne, 10 Septemba 2013

UFAFANUZI WA TAG KUHUSU ENEO ALILOZIKIWA ASKOFU KULOLA

Wakwanza kushoto ndie hayati M. Kulolawww.hakileo.blogspot.com
Ufuatao ni ufafanuzi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God kupitia askofu wake mkuu, Barnabas Mtokambali, kutokana na sintofahamu kuhusiana na mahala alipozikwa Askofu Moses Kulola, ufafanuzi huu ulitolewa tarehe 4 Septemba, ambapo Askofu Mtokambali ameeleza kuwa walichofanya ni kuweka records sawa ili huko mbeleni maafa yasije kujitokeza.

Zifuatazo ni sehemu ya nukuu alizozungumza askofu Mtokambali, unaweza pia kuisikiliza sauti yake kama ambavyo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari, ripoti ya Yaliyotokea, kipindi cha WAPO Radio FM imenukuliwa.
Mila za kiafrika mtu akizikwa pale, pale panakuwa pake. Sasa tukasema kama tukikaa kimya, hili likatokea, baadae huko mbele tutasema nini, tutajibu nini kwasababu kanisa sio langu, kanisa ni la general council, mimi nawajibika kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, kwa wachungaji wote, halafu sisi tutaondoka watakuja watoto hapa, wanataka kuchukua kanisa lao na kuna kaburi pale, wasije watu wakachinjana hapo, tupate muongozo wa kisheria, ndio hilo tu, muongozo wa kisheria juu ya jambo hili jamani isije ikatokea confusion huko mbele, lakini niwaambieni ukweli, hakuna mtu aliyefurahi kama mimi mzee Kulola kuzikwa Bugando, mimi nimefurahi saana naomba muandike, nimefurahi saana Mzee Kulola kuzikwa Tanzania Assemblies of God Bugando.


...Sasa Mzee, kwa heshima zote ameanza kazi Tanzania Assemblies of God, mwaka 68, na Mzee ameombwa na EAGT, uongozi kwa busara yao kubwa na nzuri wameona alipoanzia ndio apumzishwe, amerudishwa nyumbani – amerudishwa nyumbani baba yetu, hakukuwepo na sababu yaani mimi kama TAG, na kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, lengo letu ilikuwa ni kuweka tu record sawasawa, kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo kuzuia maafa makubwa yanayoweza kutokea baadae, lakini kamwe haikuwa hasa kuzuia, mzee azikwe pale.

Hata kesho tutakaporudishiwa lile jingo lile, tutakaporudishiwa pale mahali kumiliki asilimia 100, mtu akitaka kuja kumuondoa pale mzee nyumbani, mimi nitaweka stop order usimuondoe, utamuondoa umpeleke wapi, na mzee amelala nyumbani, nitasema jamani hapana mwacheni mzee amelala nyumbani.

Sisi tumetumia uungwana sana na uvumilivu wa hali ya juu sana, na kama kweli watu wangekuwa wanataka kuandika watu ambao kweli ni wakristo, na wameonyesha uvumilivu, tolerance ni sisi. Ni pamoja na kanisa la Temeke, ndio maana unaona pale hakuna development inayofanyika, wanajua sio petu, angalia makanisa mengine ya EAGT yanavyoendelezwa, nenda Temeke hamna kitu, hata Bugando hakuna kitu kilichoendelezwa pale, maana na wenyewe wanafahamu.

Kwa hiyo tumekuwa wavumilivu sana na tumekuwa waungwana sana, tukitarajia wenzetu.. unajua Biblia inasema mwana mpotevu akaja katika akili zake, akarudi na kusema jamani sijui mnanielewa.. na  ni makanisa mazuri tu yako kwenye very strategic place na majengo kabisa, sasa kwahiyo kutokea sasa na kuendelea, ngoja tumemaliza maziko.

Naa nashukuru Mungu nimepata taarifa, kule kwenye msiba nimetuma mwakilishi, mimi nimbeaki hapa tu kwa sababu ya ugeni wa kitaifa ambao tumeupokea hapa jana, ya kamati kuu ya kanisa la Assmblies of God kutoka Rwanda, ambao waliomba tokea mwaka jana kuja Tanzania, kujifunza namna ya ueneshaji wa kanisa.

Na tumekuwa tunapata hizi timu kutoka dunia nzima, wanakuja hapa kujifunza kama darasa, kwahiyo askofu mkuu yupo hapa na kamati yake yote imeshindikana kuondoka kwenda kwenye msiba, lakini ningekuwa kule tangu jana.


Jana tumefanya mapokezi na leo tumekuwa nao hapa, na kesho tunaendelea nao, lakini nimetuma timu kule, nimetuma askofu aliyenitangulia Mwanisongole aende msibani aniwakilishe, atoe salamu za Assemblies of God na kutoa rambirambi, naa pia amefanya kazi nzuri. Na kabla ya kuja hapa, nimeongea ne anasema shughuli zote zimekwenda vizuri, na maazishi yote yamekwenda vizuri, kwahiyo tutaendelea na huu uvumilivu lakini pia tutakaa na kuona labda wenzetu watakuwa tayari kurudi tena kwenye mapatano nje ya mahakama, sisi we are open, hatupendi vurugu, hatupendi uadui au ugomvi wa aina yoyote ule, na hatutaki kurudi tena kule tulikotoka

Jumatatu, 9 Septemba 2013

UZINDUZI WA ALBAMU YA BAHATI BUKUKU YA DUNIA HAINA HURUMA YATIKISA.

BAHATI BUKUKU AZINDUA KWA KISHINDO, MILIONI 20 ZATOLEWA NA LOWASSA


"Mtu yeyote anayeiombea amani anaipenda nchi hii. Leo natoa changamoto waimbaji wa nyimbo za injili wahubiri sana amani."

Ni kauli ya Waziri Mkuu aliyepita, ambaye pia ni mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa DVD ya album ya Dunia Haina Huruma, ya kwake Bahati Bukuku, ambayo imehudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba Jumapili hii.

THE JESUS IS KIND.

1.Brothers, my heart's desire and prayer to God for the Israelites is that they may be saved. 2.For I can testify about them that they are zealous for God, but their zeal is not based on knowledge. 3.Since they did not know the righteousness that comes from God and sought to establish their own, they did not submit to God's righteousness. 4.Christ is the end of the law so that there may be righteousness for everyone who believes.
5.Moses describes in this way the righteousness that is by the law: "The man who does these things will live by them." 6.But the righteousness that is by faith says: "Do not say in your heart, 'Who will ascend into heaven?'" (that is, to bring Christ down) 7."or 'Who will descend into the deep?'" (that is, to bring Christ up from the dead). 8.But what does it say? "The word is near you; it is in your mouth and in your heart," that is, the word of faith we are proclaiming: 9.That if you confess with your mouth, "Jesus is Lord," and believe in your heart that God raised him from the dead, you will be saved. 10.For it is with your heart that you believe and are justified, and it is with your mouth that you confess and are saved. 11.As the Scripture says, "Anyone who trusts in him will never be put to shame." 12.For there is no difference between Jew and Gentile—the same Lord is Lord of all and richly blesses all who call on him, 13.for, "Everyone who calls on the name of the Lord will be saved."
14.How, then, can they call on the one they have not believed in? And how can they believe in the one of whom they have not heard? And how can they hear without someone preaching to them? 15.And how can they preach unless they are sent? As it is written, "How beautiful are the feet of those who bring good news!"

MASANJA ASISITIZA NENO KWENYE FACEBOOK.

Masanja Mkandamizaji - Dar es Salaam, Tanzania

NA HAYA NI MANENO ALIYO YAANDIKA LEO EMANUELI MGAYA MAARUFU KWA SASA KAMA MCHUNGAJI MTARAJIWA.   ;

MUNGU WANGU NA BABA YANGU, NINAKUSHUKURU NIMEIONA SIKU MPYA YA LEO, MBELE YANGU NINAYO MAJUKUMU BABA NINAKUSIHI USINIACHE PEKE YANGU, BARIKI WAZAZI WANGU,WATOTO WANGU,NDUGU JAMAA NA RAFIKI ZANGU,YEYOTE ANAYE NIOMBEA MABAYA MIMI NINAMUOMBEA MEMA, BARIKI WOOTE WALIOKO SAFARINI WAFIKE SALAMA,BARIKI NCHI YANGU,VIONGOZI WA VYAMA NA SERIKALI,WASIO NA KAZI MUNGU WAWEZESHE,WAFANYABIASHARA BILA WEWE MUNGU HAWATAWEZA WASAIDIE,BARIKI WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WANAOJIANDAA KWA MITIHANI TUNAKATAA ROHO ZA KUFERI, BARIKI NA NDUGU ZETU WALIOKO NJE YA TANZANIA UWALINDE NA KUWATUNZA NI KTK JINA LIPITALO MAJINA YOOOTE.

Jumapili, 8 Septemba 2013

T.D JAKES AOMBEWA NA MUIGIZAJI TYLER PERRY, ROHO ATAWALA


Muigizaji, Tyler Perry akimnenea baraka Askofu T.D Jakes wa the Potter's House. ©Facebook/TD Jakes Ministries
Pata picha siku Masanja Mkandamizaji anamuwekea mkono Mwalimu Christopher Mwakasege na kumuombea, hakika wengi watashangaa na kudhani labda ni utani. Lakini la hasha, Mungu hutumia chombo chochote, hivi ndivyo ilivyokuwa Potter's House, kwenye huduma ya T.D Jakes, ambapo muandaaji (producer) na msanii muigizaji maarufu nchini Marekani na duniani kwa ujumla, Tyler Perry - alipomuwekea mkono Askofu T.D Jakes.

NDIMI ZITEMAZO KWELI!


Mimi si mwanasiasa, japo siwezi kujitenga na siasa kwani ndio mustakabali wa maisha ya mwanadamu kwenye ulimwengu wa mwili.
Ukiachilia ulimwengu wa kiroho, hivi nilivyo leo naakisi siasa za Tanzania, kwa kuwa ndizo zilizozaa sera ya elimu niliyosoma, hospitali niliyotibiwa nilipougua na sasa kazi ninayofanya. Hii ndiyo maana napata ujasiri wa kusema wazi kwamba japo si mwanasiasa lakini siwezi kujitenga na siasa.
Hoja yangu leo imejikita katika siasa, nikimulika kurunzi yangu katika ndimi za aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania), Bw. Edward Ngoyai Lowassa, pamoja na wenzake wanaotajwa sasa katika kasi ya kuwania kiti cha heshima ndani ya jumba jeupe “Ikulu”.
Kimsingi Lowassa anasura nyingi, wengine wamethubutu kumwita shujaa, na baadhi kumwita majina ambayo sina ujasiri wa kuyataja. Wanaomuita shujaa wanadai eti ni mwenye maamuzi, si mnafiki akisema ndio anamaanisha ndio, na hapana anamaanisha hapana.