Jumapili, 24 Novemba 2013

VIWANJA VYA TANGAMANO JIJINI TANGA VYAANDIKA HISTORIA MPYA

Ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano wa kanisa la Ufufuo na uzima linaloongozwa na mchungaji Josephat Gwajima unaofanyika mjini Tanga maelfu ya watu wamejitokeza katika mkutano huo na kusababisha uwanja wa Tangamano ambapo mkutano unafanyika kutokutosha maelfu ya watu hao.


Mchungaji Josephat Gwajima akifundisha katika mkutano mjini Tanga









Maelfu ya wakazi wa mji wa Tanga wakimshangilia Mungu wakati wakisimsikiliza Mchungaji Josephat Gwajima leo




Mchungaji Gwajima akihubiri mjini Tanga 


Jackson Bent akimuimbia Mungu katika mkutano wa Ufufuo na Uzima jijini Arusha



Jackson Bent akiimba mbele ya maelfu ya watu waliokuwepo katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga katika mkutano wa Ufufuo na Uzima




Wakazi wa mji wa Tanga wakiwa wamejaa mpaka upande wa barabara katika viwanja vya Tangamano mjini humo katika mkutano wa Ufufuo na Uzima



Kutoka kushoto nii Senior Resident Pastor Grace Gwajima, Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha wakiwa katika mkutano wa Ufufuo na Uzima jijini Tanga




Dada Nives akitoa ushuhuda jinsi ambavyo Bwana Yesu alimfufua kutoka kwa wafu baada ya kuombewa na mtendakazi wa Ufufuo na Uzima baada ya kufa



Ikiwa ni mara ya kwanza kwa viwanja hivyo kufurika watu wengi katika mkusanyiko wa mara moja katika historia ya uwanja huo watu walikua ni wengi mno waliojitokeza mahali hapo

Akiongea katika ufunguzi wa mkutano huo mchungaji Josephat Gwajima alifafanua kuwa watu wengi wana matatizo yanayosababishwa na viumbe wa rohoni ambao ni mashetani/majini/mapepo ambayo yanafunga maisha yao.

Mkutano huo wa utangulizi ulikua pia na shuhuda za watu ambao walirudishwa kutoka msukuleni na wengine waliofufuka kutoka kwa wafu kwa jina la Yesu.

Maelfu ya watu walifurika mpaka barabara iliyokaribu na uwanja wa Tangamano ikashindwa kupitika kutokana na maelfu ya watu waliokuja katika mkutano huo
www.mwakasegebibilia.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni