Alhamisi, 7 Novemba 2013

MWANAMAMA WA KIBAO CHA "CALVARY" SPIRIT OF PRAISE APATA MTOTO WA KIKE


Zaza akiimba kibao cha Calvary wakati wa onyesho la Spirit of Praise mwezi August mwaka huu.
Mwanamama Zanele Mokheti Mosike au mwite Zaza wa kundi la Spirit of Praise amefanikiwa kujifungua mtoto wa kike hapo jana, mwanamama huyo anayetamba kwasasa na pambio la Calvary linalopatikana katika toleo la nne la Spirit ametangaza kupata mtoto wa kike hapo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook. Mara ya mwisho kuonekana jukwaani ilikuwa mwezi wa tisa mwaka huu kisha akaamua kupumzika kutokana na hali aliyokuwa nayo.

Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 34 kwasasa na mzaliwa wa eneo linaloitwa Kwa-Thema, Springs, ameshiriki kama mwitikiaji kwa waimbaji mbalimbali akiwemo Rebecca Malope, Solly Mahlangu, Andile Majola, Keke, bila kusahau kundi la Joyous Celebration ambako aliweza kuwika kupitia wimbo wa Namhla Nkosi katika toleo la 12 la kundi hilo. Baadae akaona imetosha kuwa mwitikaji na kuamua kutoa kanda yake mwenyewe mwezi Juni mwaka 2010 aliyoipa jina la Umoya Oyingcwele ambapo mpaka sasa yupo na kundi la Spirit of Praise pia akiwa ni mwimbaji binafsi.



Zaza akiwa na Pastor Benjamin Dube, Tshepo pamoja na Omega kati ya waimbaji walioimba DVD ya nne ya Spirit of Praise.
Moja ya vitu ambavyo mashabiki wa gospel wamekuwa wakimshauri mama huyo ni kuacha kupiga kelele anapoimba, jambo ambalo muimbaji huyo amekuwa akiwaahidi mashabiki wake kuachana nalo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni