
Mzee huyu akiwa na mke wake katika madhabahu ya Ufufuo na uzima kigoma alianza kuwa mganga wa kienyeji tangu mwaka 1972 pia aliwahi kuwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondri Ujiji Kigoma. Baadhi ya kazi alizokuwa akizifanya ni kufunga mimba za wanafunzi ambao hawakuwa tayari kujifungua kwa muda huo, amesema kama mtu akimwambia anashida ya kutoa mimba, alikataa kutoa mimba bali aliweza kuizuia wala isiweze kukua mpaka wakati binti atakapomaliza masomo yake au atakapohitaji kujifungua.
Alikuwa anawavalisaha cheni kiunoni na aliwavua pindi wanapohitaji mtoto. Lakini pamoja na kuwa mganga kwa muda mrefu hakuweza kujitibu mishale iliyokuwa inayomchoma choma kifuani kwake.
leo amekuja kuombewa kanisani ufufuo na uzima kigoma akisema kwa kuwa yeye ameshindwa,,, Mungu anaweza kumponya.
Mzee huyu anaswa na majeshi ya Ufufuo na Uzima Kigoma akiionea familia yake; Anasadikika kuwa ni mchawi na alikuwa na watoto 16. Aliua mke wake "bi mkubwa" akawafanya vichaa watoto wake 3, wanne 4 walisha kufa na wengine wapo hai.
Mke wake "bi mdogo" naye akiri kuwa ndo kazi ya mume wake. J/pili 27.10.2013



Yesu ni mwema..........
Wakiwa katika madhabahu ya Ufufuo na Uzima Kigoma Albet na mdogo wake waliologwa ukichaa na baba yao mzazi, jana kaka huyu ameweza kuongea mwenyewe akishuhudia jinsi gani alianza kuumwa! Pia amesema yeye ni baba wa watoto 3 na mke wake alimkimia baada ya kuona hali yake imekuwa mbaya lakini bado anampenda na anaomba mke wake arudi maana yeye sasa ni mzima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni