Jumatano, 27 Novemba 2013

MAKALA: HUU MCHEZO UNA NIA GANI MBALI NA BURUDANI


© Desktop Nexus

Mara ya mwisho tuliona ni namna gani kuna ushabiki mkubwa hata kwa timu zinazojiita mashetani. Ninashukuru kwa wasomaji waliopata fursa ya kutuma maoni na kuelezea mtazamo wao kuhusiana na jambo hilo. Baadhi waliendelea kutoa mifano zaidi, wakifika hata kwa jogoo Liverpool, dragon wa Chelsea, majani ya Arsenal, na hata kufikia kwenye barcodes na noti tutumiazo, na kadha wa kadha, ilimradi kupinga ama kukubaliana na jambo hilo – kuwa shetani anatumia vema mambo ambayo tunayapenda kufanya shughuli yake. Hebu na tusalie kwenye mpira huu wa miguu, wengine huita kabumbu, gozi, ilimradi tu mbwembwe.
Ila kati ya waliotoa maoni yao, +Michaelm John alinikosha aliposema, "shetani ni shetani tu ata iwe kwenye mchezo ni shetani tu Mungu awafuguwe washsbiki wa soka na kifugo hiki cha kuntukuza shetani "Bwana alisema ajaribuye kuokoa maisha yake atakua anayapoteza je usemi huu kwa washabiki wa Utd wafurahishayo nafsi zao kwaushabiki watauzunisha nafsi zao jehanamu""


Lakini +Richard Laurent akatia fora aliposema "Wana masikio lakini hawasikii na wana macho lakini hawaoni...Wamepofushwa...Mungu awaondolee Mioyo ya Jiwe wapate kuelewa"


Bonyeza hapa kusoma makala ya awali na kuona mjadala ulivyoenda.


Kwa mshabiki wa mpira atakubaliana name kuwa uwanjani (kwa mashabiki) ni sehemu ambayo unaweza kusikia matusi ya kila aina, watu wanapofurahishwa ama kcuhukizwa na kinachoendelea dimbani, wakati wataalamu 22 wakipigania ushindi.


Kuna jirani yangu mmoja alikuwa akinieleza namna ambavyo ameacha kushabikia soka kutokana na vurugu ambazo hukutana nazo mara kwa mara anapoenda kutazama kibandani. Humo kuna mchanganyiko wa wenye akili zao na wasiozitumia hizo akili – vituko vya kila aina utaviona humo, na hata misemo ya kila aina utaipata humo. Huyu mara amtukane kocha (ambaye hata hatambui kama jamaa yupo) na mara huyu ampigie makofi Christiano Ronaldo (ingawa makofi yanaishia hapohapo tu).


Licha ya kuacha kutazama kwenye vibanda, pia ameacha kucheza mpira huo wa miguu kutokana na kinachoendelea viwanjani (aidha vya mazoezi ama mpambano). Kuacha kwake kunatokana na matusi mazito mazito ambayo hutolewa na vijana rika lote ambao huwepo uwanjani. Yaani imekuwa ni kama sehemu ya mchezo huo kutukana, matusi ambayo ukisikia unaweza hata kuzimia. Sasa ndio hapo ninajiuliza – ni kitu gani basi tunafaidika kutokana na mchezo huu? Ni kuboresha afya na viongo tu ama kuna la ziada lisilojulikana.



Najua michezo ni afya, na hata kupitia shule iliyokuwa chini ya mwanamichezo kanali Iddi Kipingu, naelewa hasa umuhimu wake hasa katika kuweaka akili sawa baada ya masomo, na ndio maana nilikuwa vizuri tu katika Volleyball na pia mchezo wa tennis (ndotoni).


Ila kama kila unapoenda kujenga afya unakutana na matusi na misemo ya kudhalilisha jinsia nyingine, hakika hapo hapafai. Hakuna uwepo mzuri hapo, na kazi yako kubwa ni kuwafanya wabadili mawazo yao ama uungane nao uone kuwa ni hali ya kawaida tu. Yaani matusi kila kona mithili ya sauti ya stereo ama surround.


Kwa wale ambao hushangilia vibandani, na hata kwenda uwanja wa taifa, ni lini umekuwepo uwanjani na hujasikia matusi ama maneno ya kejeli?, na huwa unajisikiaje hali hiyo inapotokea unatabasamu ama unachukia. Kwanini unatabasamu? Na kwanini unachukia? Natamani nisikie mawazo yako kwenye hili


Kwa kuangalia pande hizi mbili, kwa hakika tunaweza kuunganisha na kupata jawabu kamili, kuwa kuna jambo limejifisha katika mchezo huu, kuna jambo zaidi ya afya na burudani, na jambo hili ni kama ‘mission’ endelevu ya kuondoa ama kukondoa katika uwepo fulani. Sina nia ya kufanya juhudi za kina Jamal Malinzi na TFF zikwamishwe, la hasha. Nataka tushirikiane kudadavua hili jambo kwa pamoja.

Basi tukutane tena panapo majaaliwa, na Mungu azidi kutupa ufunuo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni