Jumatatu, 11 Novemba 2013

PRAISE POWER WAONYESHA MFANO WA DINI ILIYO BORA


Baadhi ya mali ambazo zimekabidhiwa kijiji cha wazee, Msimbazi jijini Dar es Salaam.


Wikiendi hii kuna mengi yametokea, mazuri kwa mabaya ndani yake humohumo. Kati ya zuri mojawapo, ni kitendo cha baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Redio cha Praise Power Radio kutembelea kambi ya wazee eneo la Msimbazi, jijini Dar es Salaam, na kuwapatia misaada mbalimbali kwa kadri ya uwezo wao.


Tukio hili ambalo hakika likanikumbusha kuwa kila mtu atazeeka (Kwa Neema), basi likanipa faraja nikijitazama miaka 97 ijayo, na kuona kundi la watu wakitia kambi ghafla kwenye makazi yangu kunipa maneno ya faraja na zawadi mbalimbali, inapendeza.


Gospel Kitaa ambayo ilishuhudia tukio hilo, ilipata fursa ya kumhoji meneja wa Praise Power, Bwana George Mpella, ambaye anasema kuwa msukumo wa kufanya jambo hilo unatokana na kituo chao cha Redio, yaani Faraja ya Watu , kwa hiyo licha ya kuwashauri watu kiimani zaidi, pia mwisho wa siku ni muhimu kufanya kitu kama hiki kimwili.

Kuna kinamama wana matatizo ya fistula, wakatengwa na jamii na kuna watoto wana matatizo ya kuwa na vichwa vikubwa - hawa wote wamekuwa wakipata misaada kwa namna mbalimbali, lakini ukiangalia wazee - hili ni kundi la watu waliosahaulika, ndio maana Praise Power Radio - Faraja ya Watu ikafanya jambo hilo, baada ya kufanya utafiti kujua hasa wazee hao wana uhitaji wa aina gani.

Baada ya kufanya hapa, wiki hii wanaendelea - na hapa ni kwa ajili ya wahanga wa kiafya, yaani wale waliojifungua kwa matatizo kwenye hospitali ya CCRBT. Japo hawana pesa nyingi

Mwisho wa yote Bwana Mpella anaiasa jamii ijifunze kukumbuka wasiojiweza, "sisi sote ni vijana, ila mwisho wa yote nasi tutafikia umri huo - hivyo ni vema kujifunza ni mambo gani unaweza kukutana nayo." anamaliza kusema George Mpella.


Tazama baadhi ya picha za tukio hilo kama ambavyo lilitokea.



Muimbaji Mess Jacob Chengula wa katikati akiwa na George Mpella pamoja na mtangazaji wa ppr John Kisaka





wadau mbalimbali wakifuatilia tukio hilo







Muimbaji Mess Jacob Chengula akiongoza kuimba



Maombi yalikuwa sehemu mojawapo ya siku hiyo muhimu.





Hapo kale, bibi huyu alikuwa binti, kama ulivyo mdada wewe.



Muda wa kujenga mwili ulikuwepo











Waandishi kazini, Boniphace Magupa akiwahoji wazee







Mratibu wa tukio hili, Bwana Mahunja akinena jambo wakati wa ukabidhi wa zawadi mbalimbali












Furaha katika picha ya pamoja



Mwakilishi wa GK, Silas Mbise akiwa pamoja na wadau.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni