Jumatatu, 4 Novemba 2013

NINAMWAMINIJE TENA MTU ALIYENITOSA WAKATI WA TAABU YANGU?



Na Pastor Carlos Kirimbai.
MIT. 25:19 SUV

Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.

Ngumu sana.

Yesu alisema haya maneno kwa wanafunzi wake waliyodumu pamoja naye hata katika magumu Yake.

LK. 22:28-30 SUV

Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
Wale watu wanaodumu pamoja nawe kwenye saa yako ya jaribu ndo wanaostahili kuingia nawe kwenye saa yako ya utukufu.

Magumu na majaribu yanakuja ili kukusaidia kujua umezungukwa na watu wa namna gani.

Wale wanaopita jaribio hilo ndo hasa wenye moyo wa kuwa na wewe katika safari yako ya kuelekea kwenye hatima ya Kimungu ilyoandaliwa kwa ajili yako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni