Jumatatu, 11 Novemba 2013

MUNGU BADO ANATENDA, SOMA SHUHUDA HIZI ZA KUTISHA

Soma shuhuda mbalimbali kutoka matawi ya kanisa la Ufufuo na Uzima nchini. kama zilivyotolewa katika mitandao ya kijamii ya kanisa hilo.


Ushanga aliokuwa nao mtoto huyo.
Yakikasirika majeshi, kuzimu lazima itapike watu wa Mungu iliyowameza, Ni mtoto wa miaka 11 kama uonavyo pichani alifungishwa ndoa na kuzimu na kuzaa watoto 4, Unaweza kuona ni jinsi gani shetani asivyokuwa na aibu, Bibi mzaa baba ndo alifanikisha ndoa hiyo kwa kumkabidhi mjukuu wake, pichani, pete na hereni hizo ambazo zilikuwa ndio muunganisho baina ya kijana Hussein ambaye alikuwa mume wa kijini wa binti IVONNE. Alipoletwa katika bonde la kukata maneno la Ufufuo na Uzima kwa ajili ya maombezi, Maneno yote yakakatika.



Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Ufufuo Arusha Frank Andrew kushoto akionyesha pete aliyokuwa nayo mtoto huyo.

TUKIO LA AJABU TANGAMkuu wa TANGA etekwa..

Tukiwa Mjini Tanga Leo, tukiupeleleza mji Na Mkuu wa Operation ya Saa ya Ufufuo Na Uzima, kamanda kamili wa Jeshi la Bwana, Baba yetu Josephat Gwajima, nyayo zetu zikakanyaga uwanja wa TANGAMANO ambao ndipo Mkutano Utapokitwa, kuanzia jumapili ya tarehe 24 mwezi huu, tukaona tukio la ajabu. Baada ya kuingia tu hapo uwanjani tukiwa tumepaki Gari mbali na wakaazi wengi wa mji wakifanya shughuli zao za maisha maeneo hayo, tukamwona Kijana mmoja anaelekea maeneo tuliyowaza kuweka madhabahu. Akavua nguo. Akawa Kama anabishana Na watu tusiowaona. Baba akamwendea akamuuliza unafanya nini, kijana akatoa macho Kwa hofu akijitetea, "Mzee, Mzee sio Mimi ni walee wanakimbia, mie nimekuja kujisaidia tu, Niambie nikawakamate niwalete" baba akamwambia kawalete.. Akavaa suruale Na kuondoka, hatukumfuatilia ila mara akarudi tena, Hadi tulipo Na kuanza kulalamika mwenyewe "huu uwanja ni wangu, ni wa urithi, mie siwapi ng'o " baba akamkazia macho, akaondoka akipiga kelele "Eee Mola, Walah Inshallah!, nipunguzie adhabu ya Moto wa Jehanam Kwa Sababu nimewaona Wakristo" Tulishangaa sana, amejuaje sisi ni Wakristo, uwanja Wa serikali huyu anasema ni urithi wake. Na wale aliokuwa anaongea nao ni kina nani..ni Viumbe vya Kiroho, vinajua Tanga Sasa inakwenda kutekwa. Mkutano wa Tanga utakuwa Mkubwa sana.





Mchungaji Josephat Gwajima alipotembelea Tanga hivi karibuni.
Maria John arudishwa kutoka chini ya maji ziwani Tanganyika!!
Binti huyu alifikishwa kanisani akiwa hoi hajitambui; Bila kukawia wapiganaji wazuri kabisa wa Ufufuo na Uzima Kigoma walianza kumuombea binti huyu. Wakati wachungaji wanaendelea kupigana, niliwasogelea karibu wazazi wake nijue kaanzaje kuumwa mpaka kufikia hali ambayo alikuwa nayo; Wazazi wake walidai kuwa binti yao ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kitwe Kigoma, anaumri wa miaka 16 alianza kusikia kizunguzungu akiwa darasani palepale hali ilibadilika na kupoteza fahamu ndipo walipoamua kumuwahisha Kanisani Ufufuo na Uzima Kigoma.
Baada ya kurudi binti huyu alisema kuwa alikuwa chini ya maji ziwani Tangayika tena akiwa amefungwa minyororo. Sasa ni Maria karudi kwenye mwili wake, ni mzima na minyororo hiyo ilikatika baada ya kusikia sauti inamuita "Maria njoooooooooooooo"

Maria .


Maria akifanyiwa maombi mazito kurudishiwa ufahamu na kila kitu kilichotekwa ndani yake.

Maoni 1 :