Jumapili, 2 Machi 2014

WANAWAKE WA KANISA LA VICTORY CHRISTIAN CENTRE WAMKABITHI MCHUNGAJI NYUMBA

Wakwanza kulia ni Mch. wa kanisa hili Aloyce Mbughi wapili ni Mam Mch. Catherini Mbughi na aliyebeba picha ni Mzee wa kanisa mama Doricas (mama DD)

Leo ni siku ya wanawake katika kanisa la Victory Christian Centre lilopo  hapa mkoani Arusha eneo la Morombo ambapo wamesherekea kwa kumkabithi mchunggaji wa Kanisa hili na familia yake nyumba.
Akipokea picha hiyo kama ishara ya kukabithiwa nyumba hiyo ambayo hivi sasa ipoo kwenye matengenezo na imefika kwenye lenta mchungaji wa kanisa hili Aloyce Mbughi amewashukuru kwa jitiada hizo nzuri na amewataka kuendelea na MOYO huo mwema.
Pamoja na mengi sherehe hizo zimepambwa na mashahiri mazuri na maigizo yenye kuijenga jamii KIROHO.

Wakati wa ibada ya asubuhi mwalimu aliwataka wakristo kujitoa sada kwa kuhubiri njili njema kwa mataifa yote na kuwa na MOYO wa huruma dhidi ya watua ambao hawaja okoka kwani ndivyo YESU alivyofanya kwa kanisa kake.
Pia amewataka wakristo wote kuishi maisha ya mfano yaani kama barua kwani watu wengi wakristo hivi leo wamejikuta wakiishi maisha yasiyo na ushuhuda kwani masengenyo na wivu pia mavazi maovu hutajwa kwao.
Katika ibada ya mchana Mama mchungaji Catherini Mbughi amewataka wakristo hususani wakina mama kumtegemea MUNGU kwani yeye ndiye muweza wa mabo yote.
Amenukuu maneno ya MUNGU kutoka kwenye kitabu cha Isaya 49:14-16 yanayowataka wakristo kutokukata tamaa kwani MUNGU amewachora kwenye viganja vya mikono yake na kama mama mzazi anaenyonyesha huweza kumsahau mtoto mdogo anyonyae basi Mungu hawezi kutusahau sisi.
Pia amefafanua kwa kusema kwamba mkono ni raisi sana kuonekana na ndicho kiungo zaidi katika shuhuli nyingi kwa hiyo wakati wote Mungu hututazama.Pia amenukuu maneno ya Mungu katika kitabu cha Waebr 11:11 yayozungumzia Imani na kuwataka wakristo kuishi maisha ya Imani na kumtumainia Mungu kama Ayubu na Anna aliyempata Samweli japo alikumba na vikwazo kutoka kwa mke mwenze Penina.
Chama hiki cha wanawake hujulikana kwa jina la WWK yaani Wanawake Watumishi wa Kristo,Kilianzia nchini U.S.A mwaka 1925 na mwanamama Ether Calhon katika jimbo la Tekser.
Kilikuwa na maono makuu mawili moja ni kumtunza Mchungaji siku ya Shere na pili Kufungua makanisa mapya.
Katika nchi ya Tanzania kilingia mwaka 1965 katika eneo la Mbeya Itende na mkutano wa kwanza wakitaifa ulifanyika huko Mbeya 1967 ikiwa ni miaka miwili mbeleni tangu kuanzishwa.
Pamoja na maono hayo yakuanzisha chama hiki huko Marekani pia katika nchi ya Tanzania kumeongezeka ono la tatu ambalo linalenga kuwafanya wanawake wa Tanznia kuwa jeshi Halisi la BWANA.
Tazama Picha hizi za makabilaino ya nyumba hiyo na kesho nitakupa video na vionjo vya nyimbo;


Imewekwa na www.mwakasegeinjili.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni