Jumapili, 9 Machi 2014

IBADA ZIKIENDELE KATIKA MAKANISA MKOANI IRINGA LEO



Mchungaji chavala akiendelea kuhubiri katika ibada ya asubuhi ya leo kanisani hapo
Na Martha Magessa
Jamii imeagiza kuishi maisha ya uaminifu na kuacha dhambi ili kuweza kuteka Baraka za Mungu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo, Mchungaji Lukas Chavala wa Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG) Mtwivila lililopo Manispaa ya Iringa Tanzania katika ibada ya asubuhi ya leo."Ni vema kila mmoja kuishi maisha ya uaminifu na kuacha dhambi ili kupokea Baraka toka kwa Mwenyezi Mungu Kuanzi ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla, kwani maisha matakatifu ni njia moja wapo ya kupokea Baraka za Mwenyezi Mungu".

Mchungaji chavala, ameongeza kuwa maisha ya dhambi kwa mwanadamu yanamfanya kukosa mafanikio mema toka kwa Mungu na kuendelea kubaki kama halivyo hali ambayo si nzuri kwa mwamini .

Hata hivyo, ametoa wito katika jamii kuwewza kuishi maisha matakatifu nyenye uaminifu ili kuleta matunda mema katika familia na Taifa kwa ujumla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni