Jumamosi, 8 Machi 2014

ANGALIA INJILI IKIPIGWA MITAA YA LONDON USIKU WA BARIDI KALI


Halali mtu mpaka kieleweke ni moja kati ya misemo mingi ya vijana wa Kitanzania, yawezekana msemo huu unakwenda sambamba na watumishi hawa wa Mungu ambao jicho la GK imekutana nao usiku wa kuamkia leo Jumamosi, mitaa ya Brixton kusini mwa jiji la London nchini Uingereza wakipiga injili majira ya usiku na baridi kali.GK ilipowasogelea watumshi hawa ambao walikuwa wanne mmoja akiwa amesimama kwenye kiti cha plastiki huku wengine wakisemezana na wapita njia mara moja mmoja kati ya watu hao akasogea na kuuliza unaswali lolote kuhusu Mungu aliyehai tukusaidie, GK kwa tabasamu ikasema hapana nataka kuchukua picha tu kwaajili ya kumbukumbu, yule mtumishi akasema bila shaka endelea.

Imekuwa vitu vya kawaida jijini London kukuta watu wa imani mbalimbali wakisimama makundi kutangaza dini zao na kile wanachokiamini moja ya sehemu hizo ni katika bustani ya Hyde Park ambako siku za mwisho wa juma watu wa dini hujikusanya vikundi vikundi kuhubiri habari za dini zao.

Mabango ya watumishi hao.


Wenye baiskeli walisimama kuuliza maswali, pia walijibiwa.


Mike akizungumza kuwavuta watu karibu.



Mmoja wa watumishi akisemezana na mpita njia.


Kitaeleweka tu, waliowake watafikiwa na watasikia habari njema, endelea kuwakumbuka watumishi hawa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni