Jumatatu, 10 Machi 2014

MIHADHARA YA KIDINI WAKRISTO NA WAISLAMU YAPAMBA MOTO LONDON

Angalia picha mbalimbali za makundi ya dini za Kikristo na kiislamu kama yalivyonaswa na jicho la GK wakiwa katika bustani maarufu ya Hyde park jijini London nchini Uingereza, yakivuta mamia ya makundi ya wapita njia ambao walikuwa wanaingia katika bustani hizo kupumzika na kuota jua.

Ambapo makundi hayo kila mmoja alikuwa akihubiri kuhusu kile anachoamini kuhusu dini yake, ambapo katika mihadhara hiyo ambayo hufanyika kila siku za jumapili, jumapili ya jana ilivuta mamia ya watu kutokana na hali ya hewa jijini London kuwa ya joto kiasi kutokana na kuwepo kwa jua.



Dada huyu si mara ya kwanza kunaswa na jicho la GK akipiga gombo mitaa mbalimbali ya jiji la London.


Hakika gombo analipiga hajali kama unamsikiliza ama unamcheka.


Anapaza sauti kwakweli, kama hukusikia watumishi hawa mdau wa GK utajitetea nini tena?


Muhubiri mwingine wa Kikristo akitoa ufafanuzi wa anachoamini juu ya Ukristo, huku waislamu wakimsikiliza.


Muhubiri wa dini ya Kiislamu akiwa amezungukwa akisikilizwa sera za dini yake.


Maswali yalikaribishwa kama unavyoona muumini wa dini ya kiislamu akimshika ili nayeye azungumze.



Wengine walikuwa wanapita wakiguswa sehemu ya wazungumzaji hao basi wanaweka kituo.


Babu bnayeye aah hakuwa nyuma kuzungumza anachoamini juu ya Ukristo kupitia dhehebu lake.




Muumini wa dini ya kiislamu akiuliza swali kwa muumini wa dini ya Kikristo anayeonekana kichwa.


Mwe dada yangu akipaza sauti kwa vijana hawa ambao walipita wakimtazama.


Kila sehemu vikundi, neno neno neno.




Makundi ya watu wa mihadhara ya kidini wakionekana kwa mbali kutokea ndani ya bustani ya Hyde Park.


sehemu ya bustani ya Hyde Park watu wakipumzika na wengine wakicheza michezo mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni