Jumanne, 25 Machi 2014

ALIYEKUWA AKIFANYA VITENDO VYA KIGANGA AJISALIMISHA KANISANI

Watu wanaojihusisha na masuala ya uganga na ushirikina wameendelea kujisalimisha kwa Yesu kufuatia maombi na neno linalohubiriwa katika kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Arusha. Hapo jana mwanadada Lightness amepeleka vifaa vyake vyote vya uganga na ushirikina kanisani hapo ili vichomwe moto kuashiria kwamba hataki kurudi tena katika kufanya vitendo hivyo.

SOMO: HUBIRINI MANENO LAINI YADANGANYAYO NA ASKOFU KAKOBE


Askofu Zachary Kakobe.
Wengi wetu tayari tunafahamu kwamba moja ya kazi zilizo kuu kabisa za ibilisi ni kudanganya. Yeye anaitwa baba wa uongo, kazi yake kubwa ni kuudanganya ulimwengu wote. ( UFUNUO 12:9 ), “…………audanganyaye ulimwengu wote, akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye”. Tangu wakati ule kazi yao kubwa ni kuudanganya ulimwengu yamkini kama ikiwezekana walimwengu wote wawe mbali na kweli. Kweli ni neno la Mungu. Kweli ni neno lote la Mungu. Kazi ya Shetani ni kuhakikisha wanadamu wote wanakuwa mbali na kweli. Atafanya juu chini kulipotosha neno la Mungu. Ikiwa neno la Mungu kwa mfano linazungumza juu ya Wokovu na Utakatifu hapa duniani.. Shetani atataka watu wafahamu kwamba haiwezekani kuokoka duniani. Atawadanganya kwamba wokovu siyo hapa duniani ni mpaka mbinguni ili wakifa wakute hakuna nafasi yoyote ya kuokoka na kujikuta wakiwa Jehanum. Shetani anajua kuwa mtu amewekewa kufa mara moja na baada ya kufa ni hukumu ( WAEBRANIA 9:27 ). Hakuna nafasi yoyote ya kusikia Injili baada ya kufa na ndiyo maana neno linasema “heri wafu wafao katika Bwana maana matendo yao yawatangulia”. Atawadanganya walimwengu ili wajue kwamba Utakatifu siyo hapa duniani ni baada ya kufa na watakatifu ni wachache tu, na wanateuliwa kwa vikao maalumu na mchakato fulani wa kutafuta watakatifu.. Baada ya mtu kufa ndipo mchakato unaanza na kuitwa mwenye heri na hatimaye vikao hivyo vitaendelea na mtu mmoja atatangaza kuwa mtu huyo ni mtakatifu wakati alishakufa. Watu wataamini hivyo wakati Biblia haisemi hivyo. Biblia inasema kwamba kila mtu anayetaka kuingia mbinguni na kukaa na Mungu milele anatakiwa kuwa mtakatifu.
( 1 PETRO 1:15-16 )

Jumamosi, 22 Machi 2014

SOMO : MAONO NA NDOTO * sehemu ya saba na nane*


Mtumishi Gasper Madumla.

Haleluya....
Nakusalimu nikikuambia;
Bwana Yesu asifiwe sana...

Leo tunaingia katika kipengele kipya kabisa kuhusu NDOTO.Maana katika siku sita zote tulikuwa tukijifunza kuhusu maono.

Wengi wametafsiri neno NDOTO kwa tafsiri tofauti tofauti,ingawa tafsiri nyingine si tafsiri sahihi. Leo tanajifunza tafsiri sahihi iliyo rahisi kabisa ya neno NDOTO.

Jumanne, 18 Machi 2014

MWIGIZAJI WA HOLLYWOOD AMPATIA RIHANNA UJUMBE KUTOKA KWA ROHO MTAKATIFU


Rihanna akijipiga picha ya mchoro(tattoo) wa msalaba aliyojichora hivi karibuni.
Mwigizaji nyota wa nchini Marekani Stephen Baldwin amemtumia ujumbe maalumu kutoka kwa Roho mtakatifu mwimbaji maarufu wa muziki wa nje ya kanisa Rihanna kutokana na wimbo wake uitwao "What Now" ambao unapatikana katika album yake iitwayo 'Unapologetic' aliyoitoa mwaka juzi.

WORSHIP IN THE TABERNACLE KATIKA PICHA

Siku ya jumapili ya tarehe 16 march, muimbaji wa nyimbo za injili Bomby Johnson alifanya kile alichokuwa akikitamani kukifanya, kwa kuaanda ibada ya kusifu na kuabudu ambayo aliipa jina la WORSHIP IN THE TABERNACLE. Ambayo ilifanyika VICTORY CHRISTIAN CENTER TABERNACLE (VCCT)
Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio jinsi lilivyo kuwa, japo kwa uchache huku waimbaji mbalimbali wakiungana na Bomby Johnson
WANAMUZIKI WALIJIPANGA VYEMA






Jumatatu, 10 Machi 2014

SOMO : KWANINI MWANADAMU ANASHINDWA KUACHA DHAMBI? NA ASKOFU KAKOBE


Askofu Zachary Kakobe.
Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe.

Mpendwa msomaji, Je umewahi kuchukua muda japo mfupi, kuwaza sababu inayowafanya wanadamu kushidwa kuacha maovu? Kila kukicha, mahakama zote nchini zinatoa adhabu kali kwa watu wanaofanya maovu mbalimbali; lakini maovu hayo hayaishi katika jamii, bali yanaongezeka. Magereza yamejaa wafungwa hata nafasi ya kuwaweka haitoshi, lakini pamoja na hayo, maovu hayaishi.

MIHADHARA YA KIDINI WAKRISTO NA WAISLAMU YAPAMBA MOTO LONDON

Angalia picha mbalimbali za makundi ya dini za Kikristo na kiislamu kama yalivyonaswa na jicho la GK wakiwa katika bustani maarufu ya Hyde park jijini London nchini Uingereza, yakivuta mamia ya makundi ya wapita njia ambao walikuwa wanaingia katika bustani hizo kupumzika na kuota jua.

Ambapo makundi hayo kila mmoja alikuwa akihubiri kuhusu kile anachoamini kuhusu dini yake, ambapo katika mihadhara hiyo ambayo hufanyika kila siku za jumapili, jumapili ya jana ilivuta mamia ya watu kutokana na hali ya hewa jijini London kuwa ya joto kiasi kutokana na kuwepo kwa jua.



Dada huyu si mara ya kwanza kunaswa na jicho la GK akipiga gombo mitaa mbalimbali ya jiji la London.


Hakika gombo analipiga hajali kama unamsikiliza ama unamcheka.

Jumapili, 9 Machi 2014

IBADA ZIKIENDELE KATIKA MAKANISA MKOANI IRINGA LEO



Mchungaji chavala akiendelea kuhubiri katika ibada ya asubuhi ya leo kanisani hapo
Na Martha Magessa
Jamii imeagiza kuishi maisha ya uaminifu na kuacha dhambi ili kuweza kuteka Baraka za Mungu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kwa ujumla.

Jumamosi, 8 Machi 2014

ANGALIA INJILI IKIPIGWA MITAA YA LONDON USIKU WA BARIDI KALI


Halali mtu mpaka kieleweke ni moja kati ya misemo mingi ya vijana wa Kitanzania, yawezekana msemo huu unakwenda sambamba na watumishi hawa wa Mungu ambao jicho la GK imekutana nao usiku wa kuamkia leo Jumamosi, mitaa ya Brixton kusini mwa jiji la London nchini Uingereza wakipiga injili majira ya usiku na baridi kali.
Wasalamu mpendwa,Mimi OSCAR SAMBA Napenda kukukaribisha katika mkesha wangu maalumu wa maombi utakao fanyika usiku wa jumamosi wa 15/3/2014 Katika kanisa la VICTORY CHRISTIAN CENTRE T.A.G.           Lipo Kwa MOROMBO nyuma ya ATM ya NMB BANK, Chini ya Mch.ALOICY MBUGH
Unalengo la kuombea ajenda kuu 4, Ikiwemo kuweka wakifu kipaji changu cha siasa na kuombea maono yangu ya kisiasa na yawanasiasa wa Tanzania yatimie sawasawa na Mapenzi ya MUNGU.

Natumaini utakaribia; AMANI YA BWANA NA IAMUWE MOYONI MWAKO. 0759859287 

Jumanne, 4 Machi 2014

KONGAMANO LA MOYO WA MWANAMKE KUANZA LEO HII LIVING WATER DSM

Kwa wale ambao wako jijini Dar es Salaam, kinadada kwa kina mama, hili ni tukio la kipekee ambalo unapata kufunguliwa kwayo, kwani kutakuwa na wazungumzaji wenye uzoefu mbalimbali kwa habari ya wakina mama, ambapo wenyeji wa kongamano la Moyo wa Mwanamke, Mtume Onesmo Ndegi na Mwalimu Lilian Ndegi, watakuwa pamoja na waalikwa kutoka mataifa tofauti tofauti barani Afrika kuzungumza juu ya mada ya Nguvu ya Maarifa katika Maisha ya Mwanamke.

Tukio hili lipo Living Water, Makuti Kawe, kuanzia leo Jumatano hadi tarehe 9 Machi, yaani Jumapili, hakuna kiingilio.

MCEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA NTEZE JOHN LUNGU AOKOKA, AWA MCHUNGAJI MAREKANI

CHANZO BIN ZUBEIRY
Na Dina Ismail, Dar es Salaam
MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Nteze John Lungu sasa amekuwa Mchungaji wa kanisa moja la kilokole nchini Marekani, imeelezwa.
Rafiki mmoja wa karibu Nteze, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Nteze aliyewika Pamba FC ya Mwanza na Simba SC ya Dar es Salaam, kwa sasa amekuwa mtumishi wa Mungu baada ya kustaafu soka.

Mtumishi wa Bwana; Mchungaji Nteze John Lungu (watatu toka kushoyo) aliyekuwa mchezaji wa timu ya Pamba ya Mwanza na Simba Sports Club ya Dar es Salaam pamoja na Watanzania wa

Jumapili, 2 Machi 2014

WANAWAKE WA KANISA LA VICTORY CHRISTIAN CENTRE WAMKABITHI MCHUNGAJI NYUMBA

Wakwanza kulia ni Mch. wa kanisa hili Aloyce Mbughi wapili ni Mam Mch. Catherini Mbughi na aliyebeba picha ni Mzee wa kanisa mama Doricas (mama DD)

Leo ni siku ya wanawake katika kanisa la Victory Christian Centre lilopo  hapa mkoani Arusha eneo la Morombo ambapo wamesherekea kwa kumkabithi mchunggaji wa Kanisa hili na familia yake nyumba.
Akipokea picha hiyo kama ishara ya kukabithiwa nyumba hiyo ambayo hivi sasa ipoo kwenye matengenezo na imefika kwenye lenta mchungaji wa kanisa hili Aloyce Mbughi amewashukuru kwa jitiada hizo nzuri na amewataka kuendelea na MOYO huo mwema.
Pamoja na mengi sherehe hizo zimepambwa na mashahiri mazuri na maigizo yenye kuijenga jamii KIROHO.

Jumamosi, 1 Machi 2014

SOMO : MAONO NA NDOTO * sehemu ya pili *


Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe...

"Itakuwa siku za mwisho,asema Mungu,nitawamwagia watu wote Roho yangu,na wana wenu na binti zenu watatabiri ; na vijana wenu wataota maono ; na wazee wenu wataota ndoto" Matendo 2:17