Jumamosi, 22 Februari 2014

WARAKA KWA FILEMONI * sehemu ya mwisho *


Mtumishi Gasper Madumla.

Bwana Yesu asifiwe...
Jina la Bwana libarikiwe...

Walaka kwa Filemoni ni kitabu kizuri sana ambacho ndani yake yapo mafunuo mengi ya kujifunza.
Ninajua ya kwamba kama utakuwa umebahatika kujifunza fundisho hili mahali hapa,
ni ukweli kabisa utakuwa umefaidi sana kwa kujua maana halisi ya walaka huu kwa Filemoni.
Maana si wengi wenye kuelewa walaka huu kwa Filemoni,wengi wanausoma pasipo kuelewa,na hata wengine wanauluka kuusoma,yaani hawausomi kabisa.

Haleluya....
Glory to God,glory to God....

Siku ya leo ni sehemu ya tatu na ni sehemu ya mwisho ya fundisho hili zuri. Tunaanza kwa kusoma :

"Kwa hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo;lakini,kwa ajili ya upendo nakusihi,kwa kuwa ni kama nilivyo,Paulo mzee,na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia."Filemoni 1:8-9

Haleluya...

Kumbuka hii;
Nalikuambia kwamba walaka kwa Filemoni ni walaka ulioandikwa na Paulo mtume kwenda kwa Filemoni mtenda kazi pamoja na Paulo.
Paulo anamuandikia Filemoni akimtaka ampokee Onesmo ambaye alikuwa mtumwa wake kabla ya Onesmo kumtoloka bwana wake Filemoni.

Onesmo alipomkimbilia Paulo aliyekuwa kifungoni,ndipo Onesmo akaokoka na kuzaliwa mara ya pili (Filemoni 1: 10)
Onesmo akajazwa nguvu za Mungu katika fundisho alilolipokea kutoka kwa Paulo mtume.

Kisha anatumwa kwa Filemoni aliyekuwa bwana wake.
Mtu huyo Onesmo alikuwa amejawa na fundisho, hivyo pale anapompelekea Filemoni barua hii,ni sawa na kusema alikuwa akimpelekea NENO LENYE UZIMA lililojaa ndani yake,(maana hakuwa Onesmo wa kawaida kama alivyokuwa mwanzo)

Lakini pia alimpelekea NENO LENYE UZIMA kupitia walaka ambao Paulo kwa mkono wake aliuandika (Filemoni 1: 19)

Oooh..
Haleluya....

Mstari wa nane (Filemoni 1:8) tuliousoma hapo juu;
tunaona Paulo akiwa na ujasiri mkubwa kabisa wa KUMUAMURU FILEMONI (to give the command ) ampokee Onesmo,lakini tazama Mtume Paulo akisema;

"Kwa hiyo,nijapokuwa nina UJASIRI katika Kristo KUKUAGIZA likupasalo;lakini kwa ajili ya upendo NAKUSIHI,kwa kuwa ni kama nilivyo,..." Filemoni 1:8-9

Paulo alikuwa ana uwezo wa kumuamuru Filemoni ampokee Onesmo lakini hakufanya hivyo,Bali alijishusha mpaka akasema;
"...nakusihi..''akimaanisha kumuomba Filemoni kwa sauti ya upole kabisa.

Ndiposa nikajifunza kuwa mnyenyekefu hata kwa watendaji kazi wadogo walio chini yetu sisi watumishi.
Maana Paulo alikuwa ni mtumishi mkubwa,lakini hakuona fahari kuwa mtu wa juu,akaamua kujishusha na kumuomba Filemoni ampokee Onesmo,maana Paulo alikuwa na ujasiri wa kumuamuru Filemoni.

Mungu atusaidie sana kupitia neno lake la leo mahali hapa,
maana sisi ndio tumekuwa wa kwanza kutoa AMRI kwa watenda kazi walio chini yetu,
utakuta mtumishi wa Mungu wa leo ndio mwenye kauli ya mwisho yaani akisema amesema pasipo ushauri wala kuhitaji mchango wowote kutoka kwa watenda kazi wake wa chini. HII NI MBAYA!

Au hata wale mabosi wenye wafanyakazi wa majumbani utakuta boss akimuamuru mtenda kazi wake wa chini juu ya mambo mengi ambayo mengine madogo madogo hata yeye mwenyewe ana uwezo ya kuyafanya.Lakini hafanyi kwa sababu tu yeye ndiye boss,
nayo hii ni mbaya!

Lakini Paulo mtume leo anatufundisha ;
HALI YA KUJISHUSHA NA KUWASIKILIZA WENGINE WALE WALIO CHINI YETU. soma tena ilo andiko;

" Kwa hiyo,nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo;lakini,KWA AJILI YA UPENDO,NAKUSIHI kwa kuwa kama nilivyo..."Felemoni 1:8-9

Oooh,kumbe!
Paulo aliweza kujishusha sababu ya pendo lililopo ndani yake.

*Hatuwezi kuwa wanyenyekevu na wasikivu kama hakuna PENDO LA KRISTO ndani yetu.

Paulo mtume anaongeza kutufundisha kiundani sana juu ya kuwasamehe na kuwapokea wale waliotukosa.
Maana Onesmo alimkosa bwana wake Filemoni lakini tunaona Paulo akijaribu kumwambia Filemoni arudishe moyo nyuma na ampokee Onesmo.

Sasa ngoja nikuulize mpendwa lakini usinijibu,jijibu mwenyewe;
*Ni mara ngapi unashindwa kuwasamehe waliokukosea?

Ni mara ngapi unamsamehe kwa upendo mtumishi wako wa ndani(house girl,or house boy)?

Ni mara ngapi umediriki kumkata mshahara mdada wa kazi,sababu ya kosa dogo kabisa?

BWANA MUNGU akusamehe sana,
maana hakuna wokovu wa namna hiyo,na kamwe Mungu hawezi kukusamehe wewe uliyeshindwa kuwasamehe wengine,maana tunasoma;
" Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu."Mathayo 6:12-13

Kwa lugha nyingine;
Yeye asiyesamehe wadeni wake basi naye hawezi kusamehewa.

Haleluya...

Ndani ya Yesu tuna uwezo wa kuwasamehe wadeni wetu,
Ndani ya Yesu tunajawa na upendo,
Na zaidi ya yote ;
Ndani ya Yesu tunaishi,tunakwenda na kuwa na uhai;
" Kwa maana ndani yake yeye tunaishi,tunakwenda,na kuwa na uhai wetu..." Matendo 17:28

Nami nakusihi mpendwa usomaye ujumbe huu,
Ikiwa bado hujampokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako,
basi wakati ndio sasa,nipigie namba hii hapa chini na BWANA atakwenda kukuhudumia ;

*Kwa huduma ya maombi na maombezi,namba ni hii moja tu,
0655-111149

MWISHO.

UBARIKIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni