Jumanne, 18 Februari 2014


Dar es Salaam. Mashabiki wa muziki wa Injili nchini wamependekeza mwanamuziki Solly Mahlangu 'Obrigado' kutoka Afrika Kusini awepo kwenye tamasha la Pasaka mwaka huu kwani mwanaumuziki huyo alifanya vizuri katika tamasha la Krisimasi mwaka jana.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema jana katika taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari kuwa wamepokea simu nyingi sana kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki huo wakitaka msanii huyo aalikwe katika Tamasha la Pasaka mwaka huu.

"Inaonekana Watanzania walifurahia sana kazi ya Solly Mahlangu mwaka jana, karibu kila anayepiga simu ya kupendekeza msanii, jina hilo lazima, sasa bado tunaendelea kupokea ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali, ambapo mpaka sasa Rebecca Malope na huyo Mahlangu wamekuwa wakipigiwa kura sana kwa waimbaji wa nje," alisema Msama.

Mahlangu ni muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa Injili Afrika ambaye pia anamudu kuimba Kiswahili kizuri kwa baadhi ya nyimbo zake.

Mbali ya kuwa maarufu katika nyimbo za Iinjili nchini mwake, Mahlanngu pia ni Mchungaji, ambapo kabla ya kuja Tanzania kwenye tamasha la Krismasi mwaka jana, alikuwa Harare, Zimbabwe ambako aliimba wimbo wake wa Kiswahili wa Mwamba Mwamba.chanzo MWANANCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni