Jumatano, 5 Februari 2014

KWA TAARIFA YAKO : MALIZIA TAARIFA ZA MWIMBAJI INJILI ALIYENUSURIKA KUWA MSUKULE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GKikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

KWA TAARIFA YAKO Mchungaji Nicodem anasema alikuwa hana huruma na wachawi hata kidogo na mpaka sasa bado anapambana nao, hali hiyo ilimfanya ampe siku thelasini (30) Baba yake mzazi aokoke la sivyo angekufa. lkn wakati huo pamoja na baba yake kuwa ni mchawi alikuwa pia ni mtumishi wa kanisa,. KWA TAARIFA YAKO Baba yake alianza kuumwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo ilipofika siku ya 28 alikuwa mahututi na ndipo alipopigiwa simu na kwenda kumuona mgonjwa huku akiwa amebeba soda. (Kama hujasoma sehemu zilizopita BONYEZA HAPA)
KWA TAARIFA YAKO Alipofika sehemu ambapo amelazwa baba yake akaaanza kumuita Baba Baba unaendeleaje Baba ndipo Baba yake akauliza wewe ni nani? akajibu mimi ni Nico nimekuja kukuona unaendeleaje lkn pia nilikuwa nakushauri ungempokea Yesu anaponya. KWA TAARIFA YAKO Baba yake alimjibu "Shut up Ng'ombe kasoro mkia mtoto mchawi wewe umekuja kunimaliza mimi hadi hospital toka nje" Madactari wakashangaa mgonjwa alikuwa amezidiwa anaongea wakaja na kumtoa Mch Nico naye akakubali kutoka nje akachukua soda aliyompelekea mgonjwa huku akisema wembe ni ule ule.

KWA TAARIFA YAKO Baba yake alifariki dunia kama alivyosema mchungaji Nico kwamba asipo okoka kwa mda wa siku 30 alizotoa basi atakufa na kweli Baba yake alikufa.KWA TAARIFA YAKOMchungaji Mwangila anasema mapambano hayakuishia hapo kwani walikuwa wamebaki makonkodi wengine watatu ambao ni Mme wa Shangazi yake, Baba yake mkubwa na Babu yake Mdogo ambao hao walipanga kumuangamiza.



KWA TAARIFA YAKO Mch Nico anasema alipewa taharifa ya msiba kijini ukiwa ni msiba wa Babu yake mwingine ambaye alikuwa pia mchawi akiitwa mzee John na aliamua kununua blangeti la kwenda kuzikia na alipofika kijijini hao wazee watatu waliuobaki walikuwa wamepanga hila ya kutaka kumuangamiza. KWA TAARIFA YAKO walipanga kumwangamiza kwa kutumia nyama pindi atakapo kula imkabe koo na kummaliza kabisa. Alipofika hapo walimpokea kwa furaha mpaka akashangaa na kumkaribisha ndani na hapo pia walikuwa wametoa maagizo kwamba Nico akifika apakuliwe nyama ale kablda ya watu wengine.


KWA TAARIFA YAKO mara baada ya kukaa ndani wakampakulia nyama na kumpelekea lkn kabda ajaanza kula akasikia sauti inamwambia kuwa "Nico hizo nyama ulizopewa sio nyama hayo ni mabomu kwemye ukoo wenu kuna uchawi unaitwa uchawi wa manyambuda , manamuua mtu akiwa anatembea au anaota moto au alikuwa analima mnamkuta amekufa, kwahiyo wameweka hiyo ukila kituli kimoja tu akitapita shingoni kitakukaba kwenye koo na wanataka wakuzalilishe mbele ya umati wa watu hapa msibani" KWA TAARIFA YAKO akaambiwa tena "Tazama mkono wako wa kulia " akawaona Babu Mdogo, Mme wa Shangazi pamoja na Baba Mkubwa wakiwa wamekaa pembeni huku mikono yao wakiwa wameshikilia shingo ili alakapo kula waminye sehemu ya koo na kumuua.

KWA TAARIFA YAKO Hapo ndipo mchungaji Nico aliposema hizi nyama abakishi mtu nakula sahani yote namaliza na naendakuongeza tena na hata kama akione kana mroho atahakikisha abakishi kitu.KWA TAARIFA YAKO akaanza kuomba kwa kunyunyuzia Damu ya Yesu na kuzitakasa pamoja na kufutilia mbali manuizo yote yaliyowekwa kwenye nyama. Mara baada ya kumaliza kuomba akaanza kula nyama na kumaliza sahani na KWA TAARIFA YAKO alirudia mara nne huku wale wazee wakibaki kumtolea macho hadi anamaliza huku yeye akijisemea moyoni mwake "Leo amli kitu nahakikisha namaliza nyama zote"

KWA TAARIFA YAKO alikula na kumaliza salama bila kudhurika na lolote hali ambayo imemfanya kuogopwa na kuheshimiwa katika ukoo wao huku wakisema huyu mtoto ni hatari sana sijui ameutoa wapi uchawi huu kwani kwenye ukoo hakuna mtu alikuwa na uchawi namna hii. KWA TAARIFA YAKO Mchungaji Nicodem Mwahangila anasema uchawi wake ameutoa kwa Yesu na kamwe hawezi kumwacha na mapambano dhidi ya wachawi popote pale atakapo kanyaga yanaendelea kama kawaida.

KWA TAARIFA YAKO Huyo ndiye Mchungaji Nicodem Mwahangila ambaye GK imekuelezea kwa sehemu maisha yake na jinsi Mungu anavyomtumia katika maombi ya vita. Pia Mchungaji Nico ni muimbaji na kwasasa ametoa toleo la pili linaitwa Hakuna Kubebwa, Zaidi wasiliana nae kwa 0756 27 30 49

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo vinginevyo tukutane wiki ijayoo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni