Jumatano, 26 Februari 2014
SOMO : MAONO NA NDOTO *sehemu ya kwanza *
Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...
Nasema,
Haleluya...
Ninakukaribisha katika fundisho zuri lenye kichwa cha habari kisemacho,MAONO NA NDOTO.
Kati ya mambo ambayo watu hutafuta kujua ufafanuzi na maana halisi kwa mambo yajayo au yaliyopita ni MAONO na NDOTO.
Hakuna mwanadamu chini ya jua asiyependa kujua maana ya maono aliyoyaona au ndoto aliyoiota.Watu wote hupenda kujua ufafanuzi na maana halisi katika ndoto na maono.
MAONO na NDOTO huchanganya watu wengi hata kushindwa kuyatofautisha. Mtu aweza kuona maono fulani lakini akasema ameota ndoto.
Au mtu anaweza kuota ndoto akasema ameona maono fulani.
Ndiposa Roho wa Bwana akanichukua na kunitaharakisha nifundishe MAONO na NDOTO.
Haleluya...
Sasa,
Fungua moyo wako ili Bwana akakuhudumie kupitia fundisho hili.
Tuanze na andiko hili;
"Itakuwa siku za mwisho,asema Mungu,nitawamwagia watu wote Roho yangu,na wana wenu na binti zenu watatabiri ; na vijana wenu wataona maono ; na wazee wenu wataota ndoto." Matendo 2:17
Andiko tulilolisoma hivi sasa linatueleza namna gani itakavyokuwa ndani ya nyakati za mwisho.
Mungu anasema wazi wazi kupitia kinywa cha mtume Petro.Anaanza kwa kusema atamwaga Roho yake kwa watu wote.
Tukio la kwanza baada ya Roho wa Mungu kuwashukia watu wake ni KUTABIRI.
Em sema ," kutabiri. "
Simply,neno kutabiri kibiblia lina maana ya kutoa unabii juu ya mambo yajayo kwa msaada wa nguvu za Roho mtakatifu.
Yeye anayetabiri,hatabiri kwa nafsi yake, wala sio kwa mapenzi yake,Bali ni Roho mtakatifu ndiye yupo kazini akiwezesha utabiri kwa kinywa cha mtumishi wake.
Kupitia maandiko matakatifu,wapo watu kadha wa kadha waliopata kutabiri baada ya kushukiwa na nguvu za Roho mtakatifu.
Mfano;
Tunasoma;
" na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu,nawe utatabiri pamoja nao,nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine ." 1 Samweli 10:6
Tukio la utabiri ni baada ya kujiliwa kwa nguvu na Roho ya Bwana,Kisha Biblia inaweka wazi kabisa ya kwamba yeye anayetabiri hubadilika na kuwa mtu mwingine.
Kuwa mtu mwingine ni ile hali ya kuhama kwa uwezo wa kibinadamu katika kila hali,na uwezo wa Bwana kuchukua nafasi
Maneno hayo ( 1 Samweli 10:6) anaambiwa Sauli mtu ambaye nabii Samweli alimpaka mafuta ya kiutumishi kwa kuongozwa na Mungu mwenyewe.
Sauli asingeliweza kutabiri kama asingelishukiwa na nguvu za Roho mtakatifu.Baada ya kujiliwa na nguvu za Mungu,Sauli akatabiri sawa sawa na neno la Mungu kupitia kinywa cha mtumishi wake Petro ( Matendo 2:17).
Mfano wa pili,ni huu;
Unakumbuka
Sauli alopomuasi BWANA MUNGU kwa kushindwa kutii sauti yake Mungu iliyomwambia aende kuwaangamiza Waamaleki wote,
(1Samweli 15:1-23)
Baada ya dhambi ya kuasi,Biblia inasema ;
" Basi,Roho ya Bwana ilikuwa imemuacha Sauli..." 1 Samweli 16:14
Ndiposa Sauli akaanza kumtafuta Daudi ili amuue.
Sasa,
Kuna kipindi ambacho Daudi alimkimbilia Samweli kujificha huko Rama ili kuiponya roho yake.Sauli akatuma kundi la kwanza kwenda kumkamata Daudi, kabla ya kundi la Sauli halijawakaribia wakina Daudi na kundi lao pamoja na Samweli aliyekuwa kiongozi wa kundi la akina Daudi.
Biblia inatuambia ;
NGUVU ZIKAWAJILIA NAO WAKATABIRI,(Kundi la Sauli likatabiri).Vivyo hivyo naye Sauli akaamua kwenda yeye mwenyewe kumkamata Daudi;
naye akatabili tena akavua nguo zake mbele ya Samweli,akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha siku ile. ( 1 Samweli 19: 18-24).
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya....
Hivyo kutabiri ni udhihirisho wa nguvu za Mungu,Udhihilisho unaomfanya mtu wa rohoni kunena habari ya mambo yajayo anayo yaona katika ulimwengu wa roho.
Na hilo ndio tukio la kwanza baada ya Roho wa Mungu kumwagika kwa watu wake,tukio hilo la kwanza ni KUTABIRI.
Lakini Mungu hakuishia hapo,
Anasema kwa kinywa cha Petro,kwamba baada ya kutabiri,
vijana wakiume na wakike wataona MAONO.
Tena Mungu hakuwaacha wazee.
Kundi la wazee nalo halikusahaulika maana anasema;
"...wazee wenu wataota ndoto" Matendo 2:17
ITAENDELEA....
Usikose kabisa fundisho lijalo,ambapo tutaanza rasmi kuchimba kiundani juu ya MAONO,na tukimaliza tutaingia katika ufafanuzi wa kimaandiko kuhusu NDOTO.
*Ninakuomba usikose kabisa.
Kwa huduma ya maombi na maombezi,pamoja na huduma ya kukata shauli yaani huduma ya kuongozwa sala ya toba ili uokoke,piga namba hii;
0655-111149
UBARIKIWE.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni